Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2015

List of selected students 2015/2016 in ST. Joseph University

Angalia hapa orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha ST. Joseph Majina Yote yako hapa Pakua Hapa Tafadhali mshirikishe rafiki yako hapo chini

Majina ya wanafunzi waliopangiwa chuo kikuu cha Dar es Salam-UDSM 2015/2016- JKN MLIMANI, DUCE na MUCE

Angalia majina hapa ya UDSM undergraduate admissions batch 1 2015/2016 Pakua Hapa ♥♥♥♥♡♡♡♡♡ Asante sana Majina round ya tatu angalia hapa Posted by Maarifa & FIKRA Yakinifu on  Monday, October 12, 2015  Tafadhali mshirikishe na rafiki yako hapo chini

Vigogo wanne watikisa Uchaguzi Mkuu

Dar es Salaam.            Mchakato wa kupata wagombea urais kutoka vyama vikuu vya siasa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 umeandika historia ya aina yake baada ya vigogo wanne kujitoa na wengine kuachia nafasi katika vyama vyao ghafla na kuzua mtikisiko. Vigogo hao ambao ni gumzo kubwa katika majukwaa ya kampeni ni mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa (2006—2008) na Frederick Sumaye (1995—2005) waliojitoa siku chache baada ya kuenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa na CCM kuwania urais na kujiunga na Chadema, ambako Lowassa alipitishwa kuwa mgombea urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Kupokewa kwa Lowassa na viongozi wa Ukawa (Chadema, CUF, NCCR – Mageuzi na NLD), kulitarajiwa kuwapa faraja wanachama wao lakini kumesababisha mtikisiko mkubwa baada Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu wadhifa wake akidai nafsi imemsuta na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuachia wadhifa huo na kutangaza kujit

Gwajima amjibu Slaa, amuonya asitumike

Dar es salaam .  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amejitokeza leo na kujibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa wiki moja iliyopita. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Askofu Gwajima amekanusha tuhuma za kuwa alimwambia Dk Slaa kuwa wapo maaskofu ambao walihongwa na mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa na kuitwa mshenga wa mgombea huyo. Askofu huyo amesema kuwa hajawahi kumwambia Dk Slaa kuwa maaskofu wa Kikatoliki wamehongwa na Lowassa ili wamchague hivyo aliyoyasema Dk Slaa ni kuwachafua viongozi hao wa dini. “Dk Slaa anasingizia kuwa maaskofu 30 wamehongwa na Lowassa, hii ni kuwaondolea maaskofu kuaminika (credibility) ili waonekane kuwa hawafai” alisema Gwajima na kuongeza kuwa “ Maaskofu wakatoliki hawakupewa rushwa, maaskofu wa KKKT hawakupewa rushwa, mimi sikupewa rushwa’’ Wakati Dk Slaa anatangaza kustaafu siasa Septemba Mosi, alimwita kiongozi