Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2015

Njia 10 Zinazotumika Kukwepa Kodi Bandari ya Dar es Salaam

Wakati Serikali ikikunjua makucha yake dhidi ya wote waliohusika katika kashfa ya kupitisha makontena 349 kwenye Bandari ya Dar es Salaam bila ya kuyalipia kodi, imefahamika kuwa idadi hiyo ya makontena ni sehemu ndogo tu ya mamia ya mizigo yanayovushwa kinyemela kila uchao na kuikosesha serikali mabilioni ya fedha. Hata hivyo, wakati serikali ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake, Kassim Majaliwa, ikiendelea kutafuta suluhu ya kudumu kuhusiana na ukwepaji kodi, imebainika kuwa kazi hiyo siyo lelemama kwani zipo njia zaidi ya tisa zinazotumiwa kukwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam. Mosi , ni kupitia mwanya utokanao na mfumo wa zamani wa malipo usiohusisha ule wa sasa wa kielektroniki, maarufu kama ‘E-Payment’.   Kwamba, wafanyabiashara wengi hutumia mfumo huo wa zamani unaohusisha matumizi ya karatasi zilizojazwa kwa mkono na hivyo kuwezesha ujanja wa kubadili taarifa kwa manufaa ya mitandao ya wakwepaji wa kodi. “Tatizo lililopo ni kwamba mfumo wa E

Serikali Yazungumzia Tishio la Marekani Kusitisha Misaada Tanzania

Serikali imezungumzia tishio la Serikali ya Marekani la kusitisha misaada kwa Serikali ya Tanzania kutokana na mgogoro wa kisiasa Zanzibar na kukamatwa kwa maofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Ofisi ya Ikulu jana ilisema masharti yaliyotolewa na Serikali ya Marekani yanatekelezeka na yatamalizwa kabla ya kikao cha Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Milenia (MCC) kukaa Desemba, mwaka huu. Wiki iliyopita, Serikali ya Marekani iliitaka Serikali ya Tanzania kumaliza haraka mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar, vinginevyo upo uwezekano wa kusitishwa msaada wa zaidi ya Dola za Marekani milioni 472 (Sh. bilioni 999.4), za awamu ya pili ya fedha za MCC la nchi hiyo. Fedha hizo za MCC awamu ya pili ni kwa ajili ya kuiwezesha Tanzania kusambaza umeme na kuwaunganisha wananchi wengi katika Gridi ya Taifa na uimarishaji wa taasisi zinazohusika na na sekta ya nishati. Mambo ambayo Serikali ya Marekani iliitaka Tanzania kumaliza haraka ni suala mgo

TAIFA STARS YAING’ANG’ANIA VIBAYA ALGERIA YATOKA SARE YA 2-2 UWANJA WA TAIFA.

Wachezaji wa timu ya Taifa Stars na Algeria wakichuana vikali kuwania mpira katikati yao wakati wa mchezo wa kufuzu fainali za kombe la dunia  uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku timu hizo zikitoshana nguvu kwa kufungana magoli 2-2 na kuifanya Taifa Stars kuwa na kibarua kigumu wakati wa mchezo wa maruduano utakaofanyika Novemba 17 mjini Algers Algeria ili kusonga mbele katika michuano hiyo.Taifa Stars  inahitaji kushinda katika mchezo wake huo ili iweze kusonga mbele. Baadhi ya washangilianji wakishangilia kwa nguvu wakati wa mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Hii ni staili moja wapo iliyotumiwa na washngiliaji wa timu ya Taifa Stars katika mchezo huo. Mdau Muddy, Bariki na  marafiki zao walikuwa ni mmoja wa mashuhuda wa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars. Kikosi cha timu ya Taifa ya Algeria kikiwa katika picha ya p