Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2015

Mhubiri afungwa jela maisha Rwanda

Mahakama Kuu nchini Rwanda imemhukumu kifungo cha maisha jela mhubiri aliyehusika katika mauaji ya kimbari ya 1994. Jean Uwinkindi alipatikana na hatia ya kupanga na kushiriki katika mashambulio dhidi ya Watutsi, mahakama ilisema. Mchungaji huyo wa umri wa miaka 64, kutoka jamii ya Wahutu, ndiye mshukiwa wa kwanza wa mauaji ya kimbari kutumwa Rwanda akajibu mashtaka na iliyokuwa mahakama maalum ya UN iliyoendesha shughuli zake kutoka Arusha, Tanzania. Mahakama hiyo ilifungwa mwezi jana baada ya kuwapata na hatia watu 61 na kuwaachilia wengine 14. Uwinkindi, aliyekuwa kiongozi wa kanisa la kipentekoste viungani mwa mji mkuu Kigali, alikuwa amepinga kurejeshwa kwake Rwanda. Alisema hangepata hati Rwanda, ambayo sasa inaongozwa na Watutsi. Mawakili wake wamesema atakata rufaa uamuzi huo wa mahakama huu. “Mahakama imebaini kwamba kulitokea mauaji ya Watutsi katika milima ya Rwankeri and Kanzenze na mashambulio hayo yaliongozwa na Uwinkindi," alisema Jaji Kan

CUF Watangaza Kutoshiriki Sherehe za Mapinduzi Zanzibar....Tamko Zima Liko Hapa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Tokea yalipofanyika Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964, tumekuwa tukiadhimisha tukio hilo kubwa katika historia ya Zanzibar kila mwaka inapofika siku hiyo.  Tukio hilo kubwa ndilo lililopelekea kutangazwa kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume. Chama Cha Wananchi (CUF) kimekuwa kikishiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku hiyo kila mwaka kwa kutambua kwamba Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964 ni Mapinduzi ya Wazanzibari wote.  Malengo makuu ya Mapinduzi hayo yameelezwa na kufafanuliwa vyema kupitia Dikrii Nam. 6 ya mwaka 1964 iliyopitishwa na Baraza la Mapinduzi ambayo yanatajwa kwamba ni kuleta usawa, umoja na maridhiano baina ya Wazanzibari wote na kupiga vita aina zote za ubaguzi. Tayari tumetangaziwa kwamba kuanzia tarehe 2 Januari, 2016 kutakuwa na shughuli mbali mbali zenye lengo la kuadhimisha Mapinduzi yetu na hatimaye, kama ilivyo ada na de

Somalia yapiga marufuku Krismasi

Somalia yapiga marufuku kuadhimisha Krismasi Serikali ya Somalia imepiga marufuku sherehe za kuadhimisha sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu. Mkurugenzi mkuu katika wizara ya maswala ya dini,Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa maadhimisho kama hayo yasiyofungamana na dini ya kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Al Shabab. ''Maafisa wote wa kulinda usalama wanapaswa kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yeyote yenye nia ya kuadhimisha sikukuu hiyo isiofungamana na dini ya Kiislamu.'' alisema Sheikh Mohamed Al Shabab iliua wanajeshi 5 mwaka uliopita walipokuwa wakiadhimisha sikukuu ya Krismas  Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika AU iliyoko mogadishu wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Krismasi. Wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo la kuvizia. Asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni wasilamu.

Kivazi Kifupi Chamtokea Puani Shamsa Ford

Muigizaji wa filamu, Shamsa Ford ameonja joto la jiwe hivi karibuni baada ya kuambulia matusi katika mtandao wa Instagram kutokana na kuvaa kivazi kifupi akiwa mbele ya mtoto wake wa kiume. Muigizaji huyo mahiri wa filamu ya Chausiku na Bado na Tafuta, ametoa ya moyoni kupitia mtandao huo baada ya kutukanwa na mashabiki. “ Maisha yangu hayawahusu. Ukiona hufulahishwi na chochote toka kwangu ni unfollow. Hukulazimishwa kunifollow. Yaani kuniona kwenye movie ndo mnajifanya mnanijua mpaka mnipangie maisha ya kuishi.sikilizeni nitavaa nitavyojisikia mm hata nikiamua kukaa uchi kabisaa ni mm na wala hayakuhusu. Ww subili movie Itoke ndo unikosoe. Mnaboa sana. Hebu walekebisheni ndugu zenu wanaovaa madila mchana usiku ni vyangudoa ,” aliandika Shamsa. Haya ni maoni ya mashabiki baada ya Shamsa Ford kuweka picha akiwa mevaa nguo fupi mbele ya mwanae. Salumkiemba218 : Angalia huyo mwanao asije akakutamani watoto wa sikuhizi ni shida. Annmlokole : Tembea uchi bwan

New Video:Mr Blue – Baki na Mimi (Official Video)

Cheki hapa kichupa cha ukweli sana mdau 

Watoto wa vigogo TRA wamiliki majumba mabilioni

Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Philip Mpango. KIMENUKA tena! Wakati Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ akiendelea kusimamia zoezi la kutumbua majipu katika sekta na idara za umma kote nchini, imebainika kuwa baadhi ya vigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamewamilikisha watoto wao wenye umri wa miaka mitatu hadi saba, majumba yenye thamani ya mabilioni ya shilingi, Uwazi linaripoti. TUJIUNGE NA CHANZO Chanzo makini kilicho ndani ya TRA kimeliambia gazeti hili kuwa vigogo wengi wa mamlaka hiyo, walio makao makuu jijini Dar es Salaam na mikoani, wamekuwa wakiwaandikisha watoto wao kuwa wamiliki halali wa majumba na vitega uchumi vyenye thamani ya mabilioni ya shilingi vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini. Mfano wa majumba wanayomiliki. “Wanafanya hivyo ili kukwepa mkono wa sheria kama wataambiwa kutaja mali walizonazo. Kwa hiyo unakuta jengo kama lile la… (anatajwa kigogo wa TRA anayemiliki jengo la ghorofa sita, lililopo Masaki jijini Dar) hati yake imeandikwa k

Mwanamke wa unga jela miaka 20

Anna Gemanist Mboya. Mrembo wa madawa ya kulevya ‘unga’, Anna Gemanist Mboya mkazi wa Kijitonyama, Kinondoni jijini Dar amefungwa jela miaka 20 na kupigwa faini ya shilingi milioni 148, fedha anazotakiwa kuzilipa mara atakapomaliza kifungo. Mrembo huyo ambaye ni mfanyabiashara, amefungwa Desemba, Mosi, mwaka huu mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Wilfrida Koroso kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya. Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa (pichani) amethibitisha kuhukumiwa kwa mrembo huyo na ameipongeza mahakama kwa kasi ya kuendesha kesi nyingi za madawa ya kulevya na kuzitolea hukumu. Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, Anna alikamatwa Januari 2, mwaka 2011 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kikosi kazi (task force) kilichopo katika kiwanja hicho. “Nawaomba wananchi waendelee kuwafichua wahusika wa madawa ya kulevya ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuokoa

New Video: Utanipenda (Lyric with English Translation Video), Kichupa cha ukweli sana cheki hapa

Angalia Video hapa mdau wa nguvu Sikiliza Audio hapa na Upakue Posted by Maarifa & FIKRA Yakinifu on  Saturday, December 12, 2015

Video: Real Madrid 8-0 Malmo, Ronaldo afanya mauaji

Cristiano Ronaldo akishangilia goli dhidi ya Malmo Mreno huyo alifunga magoli matatu ndani ya dakika 11kipindi cha kwanza na kuongeza jingine kipindi cha pili na kufikisha magoli 88 Ligi ya Mabingwa Cristiano Ronaldo amefunga magoli manne wakati Real Madrid ilipoiangamiza Malmo na kuufanya uwe ushindi mkubwa katika historia ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.

New video:Belle 9 – Burger Movie Selfie kichupa cha ukweli cheki hapa

Angalia hapa

Soma Habari zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 10

Tupe maoni yako hapa Mdau