Skip to main content

Taarifa Toka IKULU: Rais Magufuli Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa EU, Roeland Van de Geer na Balozi wa Israel, Yahel Vilan.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Aprili, 2017 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Geer na kuushukuru umoja wa nchi hizo kwa kutoa msaada wa Euro Milioni 205 sawa na takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo hapa nchini kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia mwaka huu.

Mhe. Rais Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo kumethibitisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na kwamba pamoja na kutoa fedha hizo umoja huo unatarajia kutoa fedha nyingine kiasi cha Euro Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendeleza viwanda, kilimo na uzalishaji wa nishati.

“Nimefurahi sana kwamba uhusiano na ushirikiano wetu unajikita kushughulikia mambo ya msingi kwa Watanzania, nakuhakikishia kuwa fedha mnazotoa zitatumika vizuri na zitatoa mchango mkubwa katika maendeleo yetu” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.

Nae Mhe. Balozi Roeland Van de Geer amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake mzuri na dhamira yake ya kujenga uchumi na kusimamia utawala bora ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, na pia amemuahidi kuwa nchi wanachama wa umoja huo zitaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Tanzania.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan na kumhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Israel hususani katika masuala ya uwekezaji, biashara, utalii na uboreshaji wa huduma za kijamii.

Mhe. Rais Magufuli amesema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua ubalozi nchini Israel na amemuomba Mhe. Yahel Vilan kupeleka ujumbe kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu kuwa Tanzania itafurahi kuona Israel inafungua ubalozi wake hapa nchini.

“Naamini uhusiano na ushirikiano wetu utaongeza manufaa zaidi kwa nchi zetu na watu wake, nimefurahishwa sana na taarifa kuwa watalii wataanza kuja kwa ndege moja kwa moja kutoka Tel Aviv Israel na hivi karibuni ndege yenye watalii zaidi ya 200 itakuja nchini kwetu, nawakaribisha sana watalii na wawekezaji kutoka Israel” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Yahel Vilan pamoja na ujumbe wake amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa wamefurahishwa na ziara waliyoifanya hapa nchini iliyowawezesha kukutana na viongozi mbalimbali na ameahidi kuwa Serikali ya Israel itajenga jengo la wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkoani Dodoma kuanzia mwishoni  mwa mwaka huu.

Mhe. Balozi Yahel Vilan amemhakikishia Mhe. Rais Magufuli kuwa Israel itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda, kilimo na kuimarisha huduma za matibabu kwa wananchi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Aprili, 2017

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

VIDEO MPYA: AMANI - KIZUNGU ZUNGU

Angalia hapa

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.