Wakati Serikali ikikunjua makucha yake dhidi ya wote waliohusika katika kashfa ya kupitisha makontena 349 kwenye Bandari ya Dar es Salaam bila ya kuyalipia kodi, imefahamika kuwa idadi hiyo ya makontena ni sehemu ndogo tu ya mamia ya mizigo yanayovushwa kinyemela kila uchao na kuikosesha serikali mabilioni ya fedha. Hata hivyo, wakati serikali ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake, Kassim Majaliwa, ikiendelea kutafuta suluhu ya kudumu kuhusiana na ukwepaji kodi, imebainika kuwa kazi hiyo siyo lelemama kwani zipo njia zaidi ya tisa zinazotumiwa kukwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam. Mosi , ni kupitia mwanya utokanao na mfumo wa zamani wa malipo usiohusisha ule wa sasa wa kielektroniki, maarufu kama ‘E-Payment’. Kwamba, wafanyabiashara wengi hutumia mfumo huo wa zamani unaohusisha matumizi ya karatasi zilizojazwa kwa mkono na hivyo kuwezesha ujanja wa kubadili taarifa kwa manufaa ya mitandao ya wakwepaji wa kodi. “Tatizo lililopo ni kwamba mfumo ...
Matukio, Habari za Uhakika