Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Kitaifa

Taarifa Toka IKULU: Rais Magufuli Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa EU, Roeland Van de Geer na Balozi wa Israel, Yahel Vilan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Aprili, 2017 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Geer na kuushukuru umoja wa nchi hizo kwa kutoa msaada wa Euro Milioni 205 sawa na takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo hapa nchini kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia mwaka huu. Mhe. Rais Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo kumethibitisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na kwamba pamoja na kutoa fedha hizo umoja huo unatarajia kutoa fedha nyingine kiasi cha Euro Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendeleza viwanda, kilimo na uzalishaji wa nishati. “Nimefurahi sana kwamba uhusiano na ushirikiano wetu unajikita kushughulikia mambo ya msingi kwa Watanzania, nakuhakikishia kuwa fedha mnazotoa zitatumika vizuri na zitatoa mchango mkubwa katika maendeleo yetu” amesema Mhe. Dkt. Magufuli. Nae Mhe. Balozi Roeland Van de Geer amempon...

VIDEO: Rais Magufuli akieleza sababu ya kuvunja Bodi ya Mamlaka ya Mapato TRA

RAIS John Magufuli amefichua siri ya hatua yake ya kuitumbua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Amesema alilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya bodi hiyo kuidhinisha Sh bilioni 26 kupelekwa kuwekwa kwenye akaunti maalumu( Fixed Account)  katika benki kadhaa za biashar [post_ads]

Tanzania's modern trailblazing bulldozer

Dr John Pombe Magufuli’s re-jigged anti-corruption machinery began this week with extra hydraulic turbo, a new blade and ripper, writes Victor Kgomoeswana. Tanzania was in the clutches of German-British colonial dealings when the first bulldozer was invented by James Porteous in 1884. Equipped with a blade in front - to push objects, rubble and soil, with a ripper in the back to loosen hard surfaces - this invention was first used in agriculture and road construction. Tanzania's President John Pombe Magufuli - the country's brand of bulldozer. Picture: Khalfan Said.  Credit:  AP However, it soon was kitted to deliver major projects like the Panama Canal's construction, and in World War I. Seventy-six years later, Tanzania's fifth president, Dr John Pombe Magufuli, was born - the country's brand of bulldozer. Nicknamed The Bulldozer’ for his disdain of sloppiness and in-exertion, he's gathering momentum in his crusade to lift Tanzania from its 117th p...

Taifa stars uso kwa uso na Super Eagles.

Charles Boniface Mkwasa Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa Julai 26, 2016 anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Mkwasa amesema lengo la kambi hiyo itakayoanza Agosti mosi, 2016 ni kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji kabla ya kuita kambi nyingine rasmi wiki ya mwisho ya Agosti kujindaa na mchezo dhidi ya Super Eagles ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Lagos Septemba 2, mwaka huu. Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili. Taifa Stars mpaka sasa ina pointi moja wakati Chad ikijiitoa katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za Tanzania...

Sidhani kama kuna mtu hata mmoja atasalimika kwenda jela’- Waziri Mwakyembe

Dk. Harrison Mwakyembe July 21 2016 Waziri wa katiba na sheria, Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 cha clouds TV na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu katiba na sheria na hili sakata la Richmond likagusiwa. Mtangazaji wa clouds TV, Hudson Kamoga alimuuliza Waziri mwakyembe kuhusiana na sakata la Richmond wakati akiwa mwenyekiti wa kamati iliyokuwa inachunguza sakata hilo ambapo walikuja na ripoti ambayo ilipelekea aliyekuwa Waziri mkuu kwa wakati huo, Edward Lowassa kujiuzulu. Hudson ametaka kujua kama kuna mambo ambayo watanzania hawakuyajua kuhusu sakata la Richmond Waziri Mwakyembe amesema ….>>>‘kesi ya Richmond tuliifanya kwa roho safi na kwa kupiga magoti kwa Mungu na tuliifanya haki kwa kila mtu tulichoamua hata tuamue kesho asubuhi nirudie tena hata koma haitabadilika itakuwa vilevile na mimi nitafurahi sana’  >>>’chini ya kanuni tunaruhusiwa kuifufua tena Richmond ili ichunguzwe upya na ninaaapa...

Taarifa kutoka Ikulu: Uamuzi wa China kuhusu ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa Tanzania

Kushoto ni Dkt. John Pombe Magufuli na Kulia ni  Bw. Liu Liang Benki ya Exim ya China imekubali kutoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Bilioni 7.6  sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za kitanzania kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kati hapa nchini kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) unaotarajiwa kuanza katika mwaka huu wa fedha. Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Liu Liang amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 20 Julai, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, kuwa pamoja na kutoa fedha hizo zitakazofanikisha ujenzi wa kilometa 2,190 za reli ya kati benki hiyo itashirikiana na Tanzania  katika kubadilishana uzoefu na utaalamu katika ujenzi na uendeshaji wa reli. Pamoja na kukubali kutoa fedha hizo, Rais huyo wa Benki ya Exim ya China amempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa dhamira ya dhati ya kuiletea nchi maendeleo ikiwemo kuharakisha ujenzi wa ...

Waziri Mkuu Aweka Jiwe La Msingi La Upanuzi Na Ukarabati Uwanja Wa Ndege Dodoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kutenga eneo la bandari kavu ili mkoa huo uweze kupokea na kuhifadhi mizigo na kurahisisha biashara kwa mikoa jirani. Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Julai 20, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa awamu ya kwanza ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wa  ndege wa Dodoma. “Ninazo taarifa kuwa Benki ya Dunia kupitia shirika la Local Investment Climate (LIC) tayari wametenga fedha kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kujenga bandari kavu na tayari fedha hizo zimeshapokelewa na Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kazi hiyo.” “Uzuri wa mkoa wa Dodoma kuna reli. Kwa hiyo makontena yanayoenda Burundi na mahali  kwingine yatashushwa hapa na kukaa kwenye bandari kavu; hivyo, wafanyabiashara watachukua mizigo yao hapa badala ya kupata shida ya kuyafuata Dar es Salaam kama ...

Serikali Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Uhaba wa Mafuta ya Petrol na Taa Hapa Nchini

Share To:             MAMLAKA ya Udhibiti ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuna akiba ya kutosha ya mafuta ya aina mbalimbali yanayoweza kutumika kati siku 13 hadi 39 nchini. Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana katika mkutano na wadau wa sekta ya mafuta nchini wa kupokea maoni juu ya mfumo wa uingizaji wa mafuta nchini. Tamko la EWURA limekuja kukiwa na tatizo la uhaba wa mafuta ya petrol, dizeli na mafuta ya taa katika baadhi ya mikoa hali iliyosababisha wananchi wa mikoa iliyokumbwa na tatizo hilo kupata adha. Ngalamgosi alisema akiba ya mafuta ya ndege iliyopo inatosha kutumika kwa siku 30 kwa nchini nzima, petroli ni zaidi ya siku 12, dizeli ni zaidi ya siku 15, mafuta ya taa ni zaidi ya siku 16, mafuta ya viwandani ni zaidi ya siku 39 na mafuta ya migodini zaidi ya siku 13. Alisema sababu ya kutokea uhaba wa mafuta unaoonekana sasa ni kuwepo kwa sikukuu zilizofulu...

Makonda Apiga Marufuku Kuvuta Sigara Hadharani......Pia Kapiga Marufuku Kuvuta Shisha

Share To:               Baada ya kutangaza vita dhidi ya mashoga juzi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana alitangaza vita nyingine; hataki uvutaji shisha akisema inachanganywa na vilevi vinavyoharibu vijana.  Makonda, ambaye alikuwa akihutubia Tamasha la Vijana lililoandaliwa na Upendo Media Group kwenye Uwanja wa Taifa aliagiza wavuta shisha hadharani, sigara na mashoga wakamatwe ndani ya siku saba.  “Ni marufuku biashara ya shisha kwenye mkoa wangu. Wanaofanya bishara hiyo wote nitawakamata. Mimi ndiye mbabe wa vita,”  alisema Makonda na kuongeza:  “Nina imani watakuwa wamefungasha virago vyao iwe ni kwenye klabu au baa maana humo wanachanganya vitu vingi; bangi na vilevi ambavyo vina madhara.”  Alisema vijana wa vyuo na sekondari ndiyo waathirika wakubwa wa kilevi hicho, ambacho huvutwa kwa njia ya bomba la mpira linalotoka kwenye jiko maalumu ambalo tumbaku huunguzwa na kutoa moshi...

CAF yaipa raha Yanga

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limemthibitisha beki Hassan Kessy kuchezea Yanga katika michuano ya Kombe la CAF CC hatua ya makundi. Licha ya Kessy pia CAF imetuma leseni ya wachezaji wengine watatu wa Yanga walioongezwa kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) hatua ya makundi, ambao ni Vincent Andrew ‘Dante’, Benno Kakolanya na Juma Mahadhi. Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema jana kuwa tayari leseni hizo zimetoka kwa ajili ya wachezaji hao kuitumikia Yanga kuanzia Jumapili ambapo itacheza na Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria. Mchezo huo wa kwanza hatua ya makundi utafanyika Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria. “Ni kweli tumepokea leseni za wachezaji wanne wa Yanga walioongezwa katika hatua hii, hivyo wote wapo huru kucheza michuano ya kimataifa kuanzia sasa,” alisema Lucas. Wachezaji hao walijiunga hivi karibuni, ambapo Kakolanya amesajiliwa kutoka Prisons ya Mbeya, wakati Kessy ...