Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kisiasa

Donald Trump akubali uteuzi wake

Donald Trump ameahidi kukomesha matukio ya uhalifu na vurugu nchini Marekani endapo atafanikiwa kuwa rais mteule wa taifa hilo, ahadi hii ameitoa kwatika hotuba yake wakati alipokuwa anathibitisha ukubalifu wake wa kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican. Maneno ama ahadi hiyo imo katika moja ya kifungu cha hotuba yake hii ni baada ya kuvuja kwa hotuba hiyo na kudakuliwa na wataalamu wa udakuzi na kueleza kuwa hotuba hiyo imesheheni ahadi tele za ya kurejesha utawala wa sheria , ikiwemo suala la kukabiliana na uhamiaji haramu na kwamba suala hilo ataliingiza katika sera za kigeni za Marekani. Image copyright GETTY Pamoja na hayo Trump anatarajiwa kutoa tamko kuwa mara moja atahakikisha anasimamia suala la wahamiaji haramu kutokana na mataifa kuathiriwa na wimbi la masuala ya ugaidi na kusisitiza ahadi yake ya kujenga ukuta kwenye mpaka baina ya Marekani n a nchi ya Mexico ili kuondokana na suala la wahamiaji. Naye mpinzani wa Donald Trump bibi...

Ted Cruz jeered, wife escorted out at raucous Republican convention

U.S. Senator Ted Cruz refused to endorse Republican presidential nominee Donald Trump at the party's convention on Wednesday, sparking an eruption of angry jeers from Trump supporters and shattering the facade of party unity that has been carefully built up in Cleveland this week. Anti-Trump Republican delegate Ken Cuccinelli told Reuters he escorted Cruz's wife, Heidi, off the floor of the Republican National Convention out of concern for her safety. Cruz, who came in a distant second behind Trump in the race for the nomination, stopped short of endorsing Trump after a bitter and personal campaign and mentioned him only once, drawing boos and repeated chants of "We want Trump." Cuccinelli said: "During the course of the speech, more and more people were coming down closer and closer to Heidi and (Ted Cruz's father) Rafael. ... When the speech ended, there was an ugly crowd behind us. ... She was trying to leave." A witness said one ...

Profesa Lipumba Atangaza Kurejea Kwenye Nafasi yake ya Mwenyekiti wa CUF.........Amwandikia Barua Katibu Mkuu wa Chama Hicho Kuomba Atengue Kujiuzulu Kwake

HATIMAYE Prof. Ibrahim Lipumba, aliyekuwa Mwenyekti wa Chama cha Wananchi (CUF) ametangaza kurejea kwenye nafasi yake ya uenyekiti-taifa wa chama hicho. Amesema, anarejea kwenye nafasi hiyo baada ya muda wa kutosha alioutumia kutafakari siasa za nchini na namna demokrasia inavyokanyagwa na watawala wa nchi hii. “Nimemwandikia Katibu Mkuu (Maalim Seif Sharif Hamad) kutengua barua yangu niliyoandika 5 Agosti mwaka jana,”  amesema Prof. Lipumba. Prof. Lipumba alijiuzulu nafasi yake mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na uamuzi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumridhia Edward Lowassa kupeperusha bendera ya umoja huo kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 kupitia Chadema. Hata hivyo amesema, analazimika kurejea kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa kutokana na kuguswa na matatizo ya demokrasia nchini. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam amesema kuwa, amemuandikia barua Maalim Seif ili atengue uamuzi wake...

Chadema kupinga marufuku ya mikutano mahakamani

Chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimesema kuwa kitaenda mahakamani kupinga tangazo la hivi karibuni la polisi kwamba mikutano yote ya hadhara inyofanywa na upinzani imepigwa marufuku. Kulingana na gazeti la Citizen nchini Tanzania, uamuzi huo wa kwenda mahakamani ulitangazwa na naibu katibu mkuu wa CHADEMA Saumu Mwalimu huko Mwanza. Inajiri baada ya mkutano wa siku mbili wa maafisa wakuu wa upinzani wakiongozwa na mwenyekiti wa kitaifa Freeman Mbowe. Gazeti hilo limesema kuwa maafisa wa Chadema na wabunge kadhaa wako katika mji huo wa Ziwa baada ya kuzuiliwa kufanya mkutano katika eneo la Kahama siku mbili zilizopita. Maafisa wa polisi walisema kuwa mkutano huo ulioshirikisha chama cha ACT-wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa kigoma Zitto Kabwe utapigwa marufuku. Na siku ya Ijumaa Bw Malimu amesema kuwa watawasilisha kesi ya kutaka kubadilisha uamuzi huo wa polisi katika mahakama kuu Mwanza.

CCM Wajibu Mapigo Zanzibar.......Wasema Uchaguzi Lazima Urudiwe

Muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kasoro na athari za kurudia Uchaguzi uliofutwa kinyume cha sheria na Jecha Salim Jecha, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametangaza kuwa uchaguzi  huo lazima urudiwe. Wakizungumza jana na vijana wa chama cha Mapinduzi katika viwanja vya Maisara waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya matembezi ya kuunga mkono Mapinduzi ya Zanzibar,viongozi wa juu wa chama hicho walisisitiza kuwa uchaguzi wa Zanzibar upo pale pale na utarudiwa kadiri tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itakavyotangaza. Wa kwanza kutoa msimamo huo alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, aliyesema kuwa uchaguzi huo utarudiwa hata ikiwezekana vyama vyote vikijitoa CCM kitashiriki peke yake “Uchaguzi wa marudio upo pale pale, tunajua uchaguzi ulifutwa kihalali, mjitayarishe kwa uchaguzi wa marudio. CUF wamesema watatumia nguvu ya umma, tunawakaribisha na wataona matokeo yake”...

KINGUNGE: MABADILIKO LAZIMA

MWANASIASA mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, jana kwa mara ya kwanza alipanda jukwaani kumnadi mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na kusema mabadiliko ni lazima. Kingunge aliyasema hayo jijini Arusha kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Sinoni. Kingunge alihutubia huku mvua ikinyesha, lakini wananchi waliokuwa eneo hilo hawakuondoka. “Historia yangu, nimeshiriki katika kuleta mabadiliko na ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kwamba kwa sasa mabadiliko katika Tanzania ni lazima, sisi t umekuwa huru kwa miaka 54 sasa. “Tulivyounda Tanu tulitaka chombo cha mabadiliko na Zanzibar  walivyounda Afro Shirazi walitaka kuwakomboa Waafrika wenzao, vyama vyote viwili vilitaka Watanzania tupate mabadiliko na baadaye kwakuwa waliamini katika mabadiliko, waliunganisha vyama na baadaye nchi, na mimi nilikuwa kwenye kamati ya watu 20 kuanzisha CCM. “CCM katika miaka ya karibuni kimekuwa na dalili ...

Steve Nyerere ametangaza rasmi anautaka Ubunge 2015, maneno yake ninayo hapa

. Aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Nyerere ameingia kwenye list ya wagombea ubunge mwaka 2015 Kwenye interview na millardayo.com Steve amesema ‘ Kwanza ninataka kuwahakikishia watanzania sijakurupuka, nimekuwa  mwanachama wa chama cha Mapinduzi  umoja wa vijana almost miaka 25 na sasa hivi nina miaka 29 naelekea 30 lakini vilevile nimekuwa kamanda wa vijana miaka 10 tawi la bwani kinondoni, nimekuwa muhamasishaji  wa chama cha mapinduzi kitaifa kwa muda wa miaka 10′ ‘Sijakurupuka na wala sijatamkia sifa kwasababu labda nimeona mtu fulani amegombea, kinondoni kuna matatizo kadhaa  nani anaweza kuyatetea hayo matatizo? nitakuwa mtetezi pamoja na matatizo ya wasanii wetu, kuhusu kazi zangu za filamu nitakuwa nafanya kama kawaida huku nikiwa natumikia kazi za Bungeni’ ATAACHA KUIGIZA?! Amejibu >>> ‘Kazi yangu ya sanaa sitoweza kuiacha nadhani naweza kuwa ndio Mbunge wa kwanza yuko ndani ya Bunge na bado yuko kw...

Video: Lowassa ajifananisha na Messi pamoja na Cristiano Ronaldo

Sumaye: Upinzani wataingia Ikulu CCM Wakipitisha mtoa Rushwa

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutopitisha mgombea  urais   kwa njia ya rushwa kwa vile  kufanya hiyo kutawaingiza wapinzani Ikulu. Sumaye ambaye ni miongoni wa makada wanaowania   kuteuliwa  na CCM kugombea nafasi  hiyo,  aliyasema hayo juzi  mjini Bariadi  alipowashukuru  wana CCM  45 waliomdhamini mkoani hapa . Akizungumza  na baadhi ya viongozi wa chama hicho  na wadhamini hao, aliwashukuru waliomdhamini na kueleza kuwa ikiwa CCM itapitisha wagombea kwa njia za rushwa utakuwa mwanzo wa vyama vya upinzani kuchukua nchi. “Nyinyi  kama wajumbe wa NEC  mtambue kuwa Tanzania kwa sasa tunahitaji kiongozi atakayetuvusha,  tukichagua kwa rushwa tunawapatia wapinzani nafasi kuingia Ikulu  hivyo chama changu kinapaswa kisipitishe mtu kwa rushwa,” alisema. Alisema sababu kubwa itakayofanya wapinzani kuongoza nchi ni rushwa n...

Mbunge Wassira Awashambulia Wagombea Wenzake.....

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira amewashambulia  watangaza  nia  wenzake  kwa  madai  kuwa  wanatumia  pesa kusaka uongozi. Alisema Tanzania inapita katika msimu mgumu kisiasa kutokana na baadhi ya watu kutumia mabilioni ya fedha kusaka uongozi wa nchi, wakati uongozi si biashara.  Wasira alitoa kauli hiyo jana wakati akiwashukuru wanachama wa CCM waliojitokeza kumdhamini katika Uwanja wa CCM Kirumba, kama sehemu ya utaratibu wa chama hicho kuelekea mchakato wa kumpata mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.  “Jamani wakati wa kujaza watu kwenye viwanja bado haujafika, mikutano ya hadhara bado.  Kwa hiyo si kwamba hatuwezi kujaza watu, tukitaka tunawez a, lakini wakati bado, utafika tutajaza watu.  “CCM na taifa kwa sasa vipo katika mazingira magumu kisiasa, rushwa sasa inainyemelea kwa kasi kubwa siasa, hii ni hatari sana, kamwe tusije ...

MAKAMBA AVUNJA REKODI YA MAPOKEZI NA UDHAMINI IRINGA

Wanafunzi wa Iringa University wakimpokea Mhe. Makamba kwa shangwe na furaha huku wakiwa wameshika mabango         Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia anayeendelea kusaka udhamini wa wananchama wenzake  ili kuingia katika kinyang’anyiro cha Urais mapema Oktoba mwaka huu, Mheshimiwa January Makamba, leo amepokelewa kwa kishindo na wanachama wa CCM Mjini Iringa na kuvunja rekodi ya udhamini ukilinganisha na wagombea waliopita. Akiongea kabla ya kumkaribisha mtangaza nia huyo anayeonekana kuwa na mvuto wa aina yake kwa vijana, Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Zongo Lobe Zongo amemtaja Mheshimiwa Makamba kuwa ni mgombea aliyevunja rekodi mkoani hapo baada ya kupata wadhamini 680 ukiachilia mbali mapokezi yenye msisimko mkubwa tofauti na wagombea waliotangulia. Akiwashukuru Mheshimiwa January Makamba, ambaye anaomba kupendekezwa na chama chake kugombea nafasi ya urais, alisema kwamba ameamua kugombea si kw...

Mbunge Nassary Aandaliwa Sherehe Jimboni Kwake, Ni baada ya Kutatua Mgogoro wa Maji

Mbunge Joshua Nassar akiwa na mkewe Anande Nnko wakati wa sherehe ya kimila iliyoandaliwa na wananchi katika jimbo la Arumeru Mashariki baada ya kufanikiwa kumaliza mgogoro wa maji uliokuwepo katika baadhi ya vijiji. Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akiwahutubia wananchi wa kata ya Leguruki na King'ori baada ya kufanikiwa kuvunjwa kwa bodi ya maji uliokuwa ikihudumia vijiji 15 katika jimbo hilo. Mamia ya wananchi wakimsikiliza mbunge Joshua Nassar wakati akizungumza katika mkutano huo.

LOWASSA APOKELEWA KWA KISHINDO MKOANI SIMIYU, APATA WADHAMINI 5,000

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akiwapungia mkono wanachama wa Chama Cha Mpinduzi (CCM) na wananchi baada ya kupokea majina ya wanachama zaidi ya 5000 waliomdhani kugombea Urais mkoani Simiyu jana. Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakicheza baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kukabidhiwa majina ya wanachama wa chama hicho zaidi ya 5000 waliomdhani kugombea Urais mkoani Simiyu. Leo  Lowassa  atakuwa  mkoani  Shinyanga  Kusaka  wadhamini.

Msanii wa bongo Movies Mchopanga Kutangaza Nia Rasmi

JUMA Chikoka ‘Chopa Mchopanga’ mwigizaji na mtayarishaji wa filamu ametangaza rasmi nia yake ya kuingia katika siasa huku akitarajia kutangaza jimbo ambalo atagombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi kwani ndio chama chake ambacho kimempatia ridhaa kugombea. “Nitaendelea kuigiza hata nikiwa Mbunge kwani lengo langu hasa ni kuwa mwanasiasa asiyeachana na Sanaa ni suala la kupanga muda tu, nitakuwa Bungeni nikipumzika lokesheni kama kawaida narekodi filamu za kuelimisha,”anasema Chopa. Msanii huyo uchaguzi uliopita 2010 aliingia katika kinyang’anyiro cha ubunge katika Jimbo la Ilala na kubwagwa chini na Mbunge wa sasa wa Ilala Mussa H.Zungu lakini Chikoka anadai kuwa maisha yake kwa sasa anawekeza katika siasa tofauti hapo awali.

Lowassa atesa kanda ya Ziwa>> Angalia Ilivyokuwa hapa

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameendelea kutesa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa anakopita kutafuta wadhamini akitafuta kuteuliwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lowassa alianza kusaka wadhamini alipotua mkoani Mwanza wiki iliyopita ambako alipata mapokezi makubwa huku maelfu ya wana CCM wakijitokeza kumdhamini. Hadi sasa Lowassa ametembelea mikoa ya Mwanza ambapo alidhaminiwa na wanachama 2676 , Geita, Mara, Mjini na Magharibi Zanzibar na Kaskazini na Kusini kisiwani Pemba. Jana aliingia Mkoa Mara akitokea Mkoa wa Geita na kupata mapokezi makubwa katika uwanja wa ndege wa mjini Musoma saa 5.00 asubuhi. Kabla hata Lowassa hajawasili Musoma, tayari watu wengi walikuwa wakimsubiri katika uwanja wa ndege, huku waendesha pikipiki (bodaboda) na magari mbalimbali yakiwa yamepangwa kwa ajili ya msafara wake. Wanachama hao walimzuia Lowassa na msafara wake aliyekuwa akienda kwenye ofisi ya CCM mkoa huku wakitaka kwanza azungumze nao. Hata hivyo, Mwenyekiti w...

Lowassa Apata Wakati Mgumu Mkoani Mara Ambako ni Nyumbani kwa Wassira........ Maelfu ya Wananchi Wazuia Msafara Wake Wakitaka Wamuone

Waziri mkuu wa zamani Mh.Edward Lowasa aliyeko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini amepata wakati  mgumu alipowasili mkoani Mara baada ya makundi ya wananchi wakiwemo vijana,wanawake na watoto   kumfuata kila alikokwenda wakitaka wapewe nafasi ya kumueleza kero zao jambo lililosababisha  zoezi la kumdhamini kuwa gumu licha ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.   Heka heka za wananchi kutaka kuzuia msafara wa Mh.Lowasa zilianza mapema asubuhi wakati  anawasili kwenye uwanja wa ndege wa musoma ambapo vijana walizuia msafara wake kutoka kwenye  uwanja huo wakitaka wapewe nafasi ya kuonana naye. Baada ya waratibu wa msafara huo kufanya kazi ya ziada ya kufanikiwa kutatua changamoto hiyo Mh.Lowasa aliekea katika wilaya ya Bunda na licha ya kusimamishwa na wananchi njiani hali  ilikuwa ngumu zaidi katika ofisi ya CCM wilaya ya  hiyo kutokana na watu kujitokeza kwa wingi. Hata hivyo pamoja na maelfu ya wananchi hao wanaounga ...

LOWASSA AZOA WADHAMINI 3,000 GEITA, CHATO

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa,(katikati), akipungia mkono  maelfu ya wana CCM na wananchi wengine waliofika kwenye ofisi za CCM wilayani  Geita Juni 8, 2015, kwa nia ya kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba  kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa  kufanyika Oktoba 25, 2015; Wakazi wa wilaya ya Geita, wakiwa juu ya nyumba na juu ya mti (picha ya chini), ili  kumuona Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa,  alipowasili kwenye ofisi za CCM wilayani Geita, Juni 8, 2015 kuomba wana CCM wamdhamini baada ya kuchukua  fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu  wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015 Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge a Monduli, Mh.  Edward Lowassa, akipokea fomu za udhamini za CCM baada ya kujazwa na  wananchama wa CCM wilaya ya Geita, kwenye ukumbi wa CCM wilayani humo...