Skip to main content

Sumaye: Upinzani wataingia Ikulu CCM Wakipitisha mtoa Rushwa

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutopitisha mgombea  urais   kwa njia ya rushwa kwa vile  kufanya hiyo kutawaingiza wapinzani Ikulu.

Sumaye ambaye ni miongoni wa makada wanaowania   kuteuliwa  na CCM kugombea nafasi  hiyo,  aliyasema hayo juzi  mjini Bariadi  alipowashukuru  wana CCM  45 waliomdhamini mkoani hapa .

Akizungumza  na baadhi ya viongozi wa chama hicho  na wadhamini hao, aliwashukuru waliomdhamini na kueleza kuwa ikiwa CCM itapitisha wagombea kwa njia za rushwa utakuwa mwanzo wa vyama vya upinzani kuchukua nchi.

“Nyinyi  kama wajumbe wa NEC  mtambue kuwa Tanzania kwa sasa tunahitaji kiongozi atakayetuvusha,  tukichagua kwa rushwa tunawapatia wapinzani nafasi kuingia Ikulu  hivyo chama changu kinapaswa kisipitishe mtu kwa rushwa,”alisema.

Alisema sababu kubwa itakayofanya wapinzani kuongoza nchi ni rushwa ndani ya CCM aliyoeleza kuwa imekithiri kwa kiwango kikubwa hasa kwa sasa kuelekea  kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

“Sijatoa rushwa tangu nianze kutafuta wadhamini , watu wanajitolea tu kwa mapenzi yao kunidhamini sina haja ya kuwanunua watu ninaowapata nawashukuru kwa maana mapenzi yametoka kwao kunidhamini siyo kwa sababu fulani, ”alisema.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

New Video: Matunzo Zero Unit Ft.Young Killer – Furaha Yetu

Angalia hapa video mpya ya Matunzo zero unit wakimshirikisha Young Killer wimbo unaitwa ‘Furaha Yetu’ Angalia hapa  na  Download