Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Gossip

Wema Sepetu kaamua kumuandikia ujumbe huu Idris Sultan

Mrembo  Wema Sepetu  ambaye jina lake July 11 2016 liliingia kwenye headlines baada ya kutoa viatu vyenye brand ya jina lake, ameingia tena kwenye headlines baada ya kuamua kumuandikia ujumbe  Idris Sultan  ambaye ni mpenzi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram. Wema Sepetu  na  Idris Sultan  kulikuwa na tetesi kuwa hawapo katika maelewano mazuri lakini usiku wa July 11  Wema Sepetu  aliamua kuandika ujumbe kupitia ukurasa wake instagram uliyolenga kudhihirisha furaha yake kuwa na  Idris Sultan . “Having you as a friend, a brother, a lover & ofcourse a shoulder to cry on everytime Im at my worst has been the best feeling ever… I wouldnt want to lose this feeling over anything… I realised Without u then I aint complete…. You have stood by me in good tyms and bad, & even when I messed up soooo bad you would look me in the eyes and tell me, “Baby, its okay, we gon fix this”… Idris you have been one of a kind and ...

EXCLUSIVE: Aunty Ezekiel Kaelezea Siku Mose Iyobo Alipohisi Mtoto Sio Wake

Mwigizaji Aunty Ezekiel amekaa kwenye Exclusive ya AyoTV na kuelezea vitu kadhaa kwenye mapenzi yake na Dancer wa Diamond Platnumz  Mose Iyobo ambapo miongoni mwa alivyoongelea ni pamoja na siku ambayo Mose alihisi ujauzito aliokua nao Aunty sio wa mtoto wake. ‘Kwanza Mose Iyobo aliniambia niitoe hii mimba nilipomuuliza kwanini akasema najua wewe Aunty Ezekiel huwezi kuzaa na mimi, akaniambia hajajipanga sababu ana mtoto mwingine, nilimwambia hii mimba ni yangu na kila afanye maisha yake kama ni hivyo….‘ – Aunty Ezekiel

Nuh Mziwanda: Sina mpango wa kufuta Tattoo ya shilole ila nimesikitika kwa sababu amefuta yangu.

Msanii Nuh Mziwanda amedai mbali ya kuachana na Shilole lakini hana mpango wa kufuta tattoo ya mrembo huyo. Nuh amesema amesikitishwa na kitendo cha Shilole kufuta tattoo yake mara tu baada ya kuachana, “Kiukweli nimesikitika sana hata kama tumeachana mimi mbona sijafuta tattoo zake na sina mpango wa kuzifuta kwa sasa”Alisema Nuh. Hata hivyo Shilole alipoulizwa kuhusiana na alichokisema Nuh alisema kuwa mbona Nuh aliwahi kuwapost mademu zake wapya mara tu baada ya kuachana. “Mimi nimewahi kufuta tattoo kwa sababu yeye alianza kuwapost mademu zake wapya Instagram baada ya kuachana” Alisema Shilole. Source: CloudsFm

Shilole Amtaja Mpenzi wake Mpya Mwanamuziki Kutoka Uganda, Adai ‘’Nuh Hanipendi"

Kwa sasa ni dhahiri kabisa penzi la Shilole na Nuh Mziwanda limefika mwisho baada Shishi kumtambulisha mpenzi wake mpya msanii,Eddy Kenzo kutoka nchini Uganda. ‘’ Nuh hanipendi Eddy Kenzo ndio ananipenda,ameniimbia wimbo nilikuwa sijui,naomba mjue kuwa ndiye mchumba wangu mpya,’ ’Alisema Shilole. ‘’ Eddy Kenzo amenipenda tangu zamani lakini nilikuwa nikimpuuzia tu maskini ameonyesha upendo wake kwangu hadi kaimba wimbo kwa ajili yangu unajua sio kitu kidogo msanii mkubwa Afrika kuniimbia wimbo mimi amechukua tuzo ya BET mwaka huu,ananipenda na mimi nampenda sana ,’’Alisema Shilole.

MSANII WA BONGO FLEVA NEY WA MITEGO ANASWA NYUMA YA BAJAJI AKIFANYA MAMBO YA KIKUBWA

YA leo siyo ya kesho! Wakati Juni 9, mwaka jana, nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki  ‘Nay wa Mitego’ alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake ‘bethidei’ kwa mbwembwe kubwa ambayo iliandaliwa na mzazi mwenzake, Siwema pale Kimara Barudi, Dar, mwaka huu ziii huku akinaswa kimahaba na Mbongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’, Ijumaa lina kila kitu. Nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki  ‘Nay wa Mitego’ akiwa na mbongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ wakiwa kimahaba. Jumanne iliyopita, Nay alijikuta akisherehekea siku hiyo bila kuwa na hekahaka ambapo mapaparazi wetu walimkuta kwenye Studio ya De Fetality ya Mensen Selekta iliyopo Sinza ya Madukani, Dar na baadaye alijikuta akiloweshwa maji na prodyuza wake, Tee Touch. Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja ndani ya studio hiyo, Nay, jioni ya siku hiyo alikuwa kwa mama yake mzazi, Kimara akiwa anajua siku imepita na hakuna cha sherehe. “Ilikuwa saa tatu usiku, Tee Touch akamuuliza aliko, akase...

Maneno ya Wema Sepetu Baada ya Kutuhumiwa Kutoka Kimapenzi na Mume wa Linah

Siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu ya kitendo cha Wema Sepetu kumchukua aliyekuwa bwana’ake Nangari Kombo, muigizaji huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria kejeli, kuwa aache presha, kwani zile ni picha tu! Wiki iliyopita zilisambaa  picha  mtandaoni zikimuonyesha Wema Sepetu akiwa amepozi kitandani na kijana huyo, aliyepata umaarufu baada ya kuingia ndani ya eneo la kuchezea katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam mwaka 2010, wakati wa mechi kati ya Brazil na Taifa Stars na kumkumbatia kiungo nyota wa mabingwa hao wa zamani wa dunia, Kaka.   Katika  maelezo yake  kuhusiana  na  kusambaa  kwa  picha hizo, Wema amesema kupiga picha na Nangari hakumaanishi mapenzi, kwani yeye ni mtu wa watu na picha kama hizo hupiga na marafiki zake wengi tu, hivyo Linah asiwe na shaka naye hata kidogo. “Nilipiga naye kama ninavyoweza kupiga na marafik...

SOMA ALICHO KIANDIKA LEO KAJALA KUHUSU WEMA NA PETITMAN>>>>HAKIKA UTAHUZUNIKA HATA WEWE

Binadamu tuliumbwa kuishi katika misingi ya ubinadamu na sio unyama kama waishivyo wanyama wa porini leo naomba kusema kutoka moyoni mwangu.. Najua kabisa nina wazazi wangu ndugu zangu na zaidi sana Mungu wangu ila kuna watu mpaka nakufa kamwe sintowasahau katika kuta za moyo wangu katika kipindi changu kigumu nilichopitia mlikuwa nembo namboni kubwa katika kuokoa maisha yangu... Napenda kusema kuwa hata kwa haya yote tunayopitia bado ni madogo sana kuficha thamani yenu mliyoijenga juu yangu. Nakumbuka sana mlipojitoa kwa ajili yangu mlipojinyima kwa ajili yangu mlipopigana kwa ajili yangu,mlivyofedheheka kwa ajili yangu yote hayo nayakumbuka na namshukuruu mungu kwani naona kabisa mliletwa duniani kwa sababu nyingi na moja ya sababu ilikuwa kuniokoa katika kipindi kigumu katika maisha yangu. Leo hii tarehe 25.5.2015 napenda kusema kwa umma na zaidi kwa Mungu wangu kuwa nawathamini nawapenda na nashukuruuu sana kwa yote mliyofanya juu yangu. Nawaombea kwa Mung...

Mfahamu Zaidi Mwigizaji Rose Ndauka....Wapi Alitoka, Lini Alianza Sanaa na Mengine Mengi Kuhusiana na Maisha Yake

Anafahamika zaidi kama Rose Ndauka ni mmoja warembo wenye mvuto wa pekee ndani ya tasnia ya bongo movies kwa vipaji vyake vingi sana.    Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza pia ose ni mwandishi na mwongozaji wa Filamu.    Akiwa ameshaigiza kwenye zaidi ya Filamu kumi na saba (17) na kupata tuzo mbalimbali ikiwemo ya best actress in mini ziff 2011; Rose Pia ni mfanyabishara na anamiliki kampuni yake binafsi iitwayo Ndauka Entertainment inayojihusha na mambo ya Filamu na burudani.    Rose Hupenda kusikiliza muziki, kuogelea, na  kusoma vitabu akiwa yupo nyumbani   Historia ya Rose inaanza tarehe saba (7) mwezi wa kumi (10) mwaka 1989. Huu ni mwaka tarehe na siku alipozaliwa.    Alizaliwa hapa hapa Tanzania na kupata elimu yake katika shule ya sekondari zanaki- Dar es salaam . Toka alipokuwa mdogo sana Rose alipenda kuigiza.   Kipaji chake Kiligunduliwa na mama yake mzazi kabla ya yeye mwenyewe kuamua kujiingiza r...

OGM! .....Irene Uwoya Releases Sexy Photos while Taking a Shower in a Bathtub

Through instagram actress Irene Uwoya shared these hot pics of herself being in a bathtub with no piece of cloth to cover her hot chest............

SHILOLE, NUH MZIWANDA WATUA UBELGIJI KUFANYA SHOO

Wanamuziki Shilole na mpenzi wake Nuh Mziwanda wametua nchini Ubelgiji jana tayari kwa shoo yao ya nguvu ya Jumamosi hii nchini Ubelgiji. Wakiwa na nyuso za furaha hotelini walipofikia wameahidi kufanya bonge la shoo kwa pamoja. Wameomba wapenzi wao wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani ya uhakika toka Bongo. Nuh Mziwanda (kushoto) akiwa na Shilole 'Shishi Baby' wakiwa tayari kuwapagawisha wapenzi wao Jumamosi hii hapo Antwerpen.

DALILI TANO MBAYA KWENYE UHUSIANO UKIONA, UJUE MPENZIO ANACHEPUKA

Leo naomba pia niongelee kuhusu dalili ambazo zinaweza onekana kwa mwenza wako ambazo zinapelekea kujenga fikra kwamba   "unasalitiwa"   dalili hizo ni kama zifuatazo:- 1.Nakupenda lakini Sina Hisia nawe(Kwa wale ambao bado hawajaoana) Hii ni dalili kwamba Mpenzi wako ana mtu mwingine nje na inawezekana kabisa kwamba yeye ndo anapendwa zaidi yako wewe hata kama muda mwingi upo nae! Anakutumia tu huyo !  2.Sisi ni Marafiki tu! Kwa ambao bado hawajaoana Ukimuuliza Mpenzio unanichukuliaje au mimi ni nani kwako anakuwa anasuasua sana sana utaambiwa ni marafiki tu.Na kwa ambao tupo katika Ndoa ukiuuliza vipi mbona nakuona una mazoea ya karibu mno na mtu fulani? Utaambiwa ni Rafiki tu!  3 Nahitaji muda wa kufikiria kuhusu hisia zangu! Hili nijibu tosha kwamba Kuna Mwenzio ambaye anamchanganya akili mpenzi wako na ndio maana anakuwa hivyo! Anza kukaa tayari au mguu nje, mguu ndani! 4.Mabadiliko ya Ratiba za Kazi Kwa wale ambao tupo ndani ya ndoa au mahusiano ya mu...

VANESSA MDEE: SASA HIVI SIWEZI KUWA NA MTOTO…

Muimbaji wa ‘Nobody But Me’ Vanessa Mdee a.k.a Vee Money ambaye hivi sasa ameweka wazi uhusiano wake na Jux ambaye ni boyfriend wake, ameweka wazi ni kipindi gani angependa kupata mtoto. Vanessa (26) ambaye muziki wake umeanza kupata njia kwenye soko la kimataifa, amesema kuwa licha ya kuwa anapenda kupata mtoto lakini kwa sasa hayuko tayari kutokana na kuwa busy kupita kiasi. “Sasa hivi sehemu ambayo nilipo katika maisha yangu niko very busy na kazi yaani, na nataka nikipata mtoto wangu au nikiwa tayari kupata mtoto niwe na uwezo wa kumlea sio kifedha tu lakini kuwepo katika maisha yake malezi ya mama yake ya karibu, akienda kulala nipo akiamka nipo kumchukua kutoka shuleni nipo, sasa hivi siwezi kufanya hivyo na siwezi kusema ndani ya miaka mitatu au minne mitano” Vee Money aliiambia Amplifaya ya Clouds Fm. Alipoulizwa kama anampenda sana Jux alijibu, “Sana, he is a great guy…he is my boyfriend”

MWANAUME WA UGANDA AFUNGUKA: ZARI AMETOA MIMBA ZANGU 2

NA SIFAEL PAUL Hasira ya kibuti? Ubuyu kutoka nyumba ya jirani, Kampala nchini Uganda unaeleza kuwa mwanaume Farouk Sempala aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameibuka na madai mazito kuwa mwanamama huyo alichoropoa mimba zake zaidi ya mbili. Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady. TUJIUNGE UGANDA Katika mahojiano maalum na Gazeti la Red Pepper la nchini humo hivi karibuni, Sempala alifunguka kuwa alishtushwa na habari kuwa mwanadada huyo alikutana na Diamond kwenye ndege na kuanza projekti ambayo matokeo yake ni mimba. MIMBA ZAIDI YA 2 Jamaa huyo alidai kuwa, wakati akiwa kwenye mapenzi na Zari baada ya mwanamama huyo kutengana na mumewe, Ivan Semwanga, alitoa mimba zake zaidi ya mbili hivyo anaamini kuwa hata hiyo ya Diamond anaweza kuichoropoa.Sempala alisema kuwa katika kipindi cha mapenzi yao, walikuwa ha...

KAULI YA WEMA YALIZA WENGI. Aweka wazi kuwa hawezi kupata mtoto.

  Kumbukeni na mimi pia ni binaadam... Nina moyo kama nyie... Au mnadhani napenda kuona wenzangu wana watoto au wana ujauzito alafu mimi sina hata wa kusingiziwa... Mnaona nafurahia sio.... Hivi mna nini jamani... Yaani mtu unaweza weka post kwa nia nzuri then people jus come from nowea wanaanza kukuandikia maneno ya kukuumiza kabisa nafsi hadi mtu unakaa unajiuliza umemkosea nini mwenyezi Mungu... Kwani kuna niliemkosea yoyote mpaka muanze tu kunikashif na kunitolea maneno mazito namna hio... Kisa mtoto... Mnadhani naipenda hii hali... Hata mimi natamani kuitwa mama na hakuna kinachoniuma kama hicho.... So mnadhani sijui kama umri unaenda na maisha yenyewe sikuhizi mafupi anytime we die... Mnafikiria nisingependa kuacha hata ka copy kangu siku ndo Mungu anasema ananichukua... Hata mimi natamani ningekuwa napiga picha niko na mwanangu... I want dat with all my life but I cant.... Sitokaa nimkufuru Mungu wangu hata siku moja maana sijui ni kitu gani kan...

PICHA ilisambaa Diva akipigwa busu jukwaani.. Crazy GK kasemaje? Msikilize kwenye #UHeARD

Hii imesikika muda mrefu, uhusiano wa Loveness Diva na Crazy GK .. minong’ono ikamfikia Soudy Brown kwamba wawili hao  wameachana kisa ni PICHA inayomuonesha Diva akipigana mabusu na star wa Bongo Fleva kwenye show. Soudy Brown amemtafuta GK  ambae amesema hakuwepo kwenye show hiyo, aliziona picha hizo kwenye mitandao na yeye aliona ni tukio la kawaida kwa sababu wote ni watu wa burudani.. ishu ya kuachana kumbe sio kweli, GK amesema bado wako pamoja kama zamani yani. Kusikiliza story yote bonyeza play hapa chini…

SHILOLE AFANYA UCHAFU MWINGINE JUKWAANI,NUH MZIWANDA AMWAGA MACHOZI BAADA YA SHISHI KUBAMBIWA>>> Bofya kusoma hapa

Shilole akizidi kupagawisha mashabiki wake. “Jamani hebu mwangalieni Shilole vitendo anavyovifanya pale jukwaani yaani dah, anajua kabisa hii shoo hata watoto wadogo wapo, hapo sijui anawafundisha nini, mimi sijapenda kabisa,” alisikika akilalamika shabiki mmoja.

DHAMBI YA PASAKA!>>>> Soma yaliyotokeo kwa undani hapa

Issa Mnally na Richard Bukos AMA KWELI duniani kuna mambo! Wakati wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, dada mmoja ambaye ni mke wa mtu yeye alijikuta akiiserebukia kwa fumanizi gesti, tena akiwa na mume wa mtu! Mwanamke aliyefumaniwa gesti akijivinjari na mume wa mtu. Tukio hilo lilijiri Alhamisi Kuu maeneo Buza jijini Dar, mishale ya saa 7:00 usiku huku jamii ikiwa katika harakati za kununua hiki na kile kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka iliyoadhimishwa duniani kote jana huku leo ikiwa ni Jumatatu ya Pasaka. ...akivaa nguo zake ili wapelekwe kituo cha polisi. Katika fumanizi hilo, timbwili la aina yake liliibuka baada ya mwanamke huyo mwenye mwili mkubwa, kuponyoka mikononi mwa mke aliyemnasa na kutoka nduki nje akiwa mtupu bila kujali hali hiyo. ...akichukua vitu vyake na kupakia kwenye mkoba tayari kwa kupelekwa kituo cha polisi. MADAI YA AWALI Awali, ilidaiwa kuwa mume huyo wa mtu aliyefahamika kwa jina la baba ...

STAA WA FILAMU BONGO.RAY AMSALITI CHUCHU KWA HUSNA, WANASWA USIKU

MUIGIZAJI  nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, amedaiwa kumsaliti mpenzi wake wa siku nyingi, Chuchu Hans baada ya kukutwa akiwa amepozi kimahaba na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011, Husna Maulid katika Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar, hivi karibuni.   Muigizaji   nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ akipozi kimahaba na Husna Maulid. Wawili hao waliokuwa wamepakatana, walikutwa katika ukumbi huo wakati bendi mbili kubwa za muziki wa dansi nchini, FM Academia na The African Stars ‘Twanga Pepeta’ zilipokuwa zikiangusha burudani kabambe ya kushindana. Uwepo wa Ray na Husna ulitafsiriwa kuwa ni usaliti kwani muda wote waliokuwa ndani ya ukumbi huo wawili hao walikuwa wamegandana kimahaba huku wataalamu wa ubuyu wakikazia madai kwa kusema wawili hao ni wapenzi.     Husna Maulid akisisitiza jambo kwa Ray. “Sasa wewe kusoma hujui hata picha huoni? Hawa watakuwa ni wapenzi tu, haiwezekani mtu mpakatane, mpeane kampani kiasi hik...

WATOTO WANASWA GEST WAKIPEANA MAMBO MAZITO, MMOJA WA DARASA LA SABA

KWELI ni watoto! Wanafunzi wawili, wa kike ana miaka 14 (darasa la saba), wa kiume miaka 15 (kidato cha kwanza) mjini hapa wanadaiwa kukutwa ndani ya gesti moja ikisemekana walikuwa na lengo la kuivunjilia mbali amri ya sita ya Mungu. Binti huyo akidhibitiwa na polisi.Tukio hilo lililojaza umati lilijiri hivi karibuni katika gesti hiyo ambayo inadaiwa haina usajili halali iliyopo jirani na soko. Habari zinasema kuwa, siku hiyo denti wa kike alitumwa sokoni na mama yake kununua mahitaji mbalimbali ya chakula lakini alichelewa kurudi.   Ikazidi kudaiwa kuwa mama yake alimfuatilia huku akiwauliza watu, ndipo mbeya mmoja akamtonya kuwa amemwona binti yake akiingia gesti hiyo na kivulana! Mama wa watu, akiwa na mshangao, naye alizama ndani na kuwakuta chumba namba 5. Kikanuka! Risasi Jumamosi lilifanikiwa kutinga eneo la tukio wakati wa sekeseke hilo na kuzungumza na mashuhuda wawili, Asha Chande na Tausi Omary.Walipohojiwa na mwandishi wetu walisema waliwaona wawili hao wakizama ndan...

AMTOROKA BWANA’KE AJIACHIA NA MIDUME 5

  BINTI aliyefahamika kwa jina moja la Ashura, anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu, hivi karibuni alimtoroka bwana’ke na kuonekana akijiachia hovyo na wanaume watano tofauti katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam kulipokuwa na onyesho la Bendi ya Taarabu ya Mashauzi Classic. Ashura, anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu akisakata ngoma. Akionekana kuwa ‘vizuri’ kichwani, kwa kiburudisho alichopata usiku mnene, binti huyo alionyesha umahiri mkubwa wa kukata mauno kiasi cha kuwavutia wanaume ambao kila mmoja alitaka kuwa naye karibu kiasi cha kumfanya kuwa bize kwa kila wimbo kulazimika kucheza na wanaume tofauti. Baadhi ya wanawake waliokuwa na waume zao jukwaani, walionyesha kukasirishwa na mwenzao huyo, kwani licha ya kuwa hodari wa kucheza, pia aliwaruhusu wanaume kumkumbatia kadiri walivyopenda, kiasi cha kusababisha wakware wengi kuwa na hamu ya kushiriki naye. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo walisema mrembo huyo alitia aibu kwani kuna wa...