Skip to main content

WATOTO WANASWA GEST WAKIPEANA MAMBO MAZITO, MMOJA WA DARASA LA SABA






KWELI ni watoto! Wanafunzi wawili, wa kike ana miaka 14 (darasa la saba), wa kiume miaka 15 (kidato cha kwanza) mjini hapa wanadaiwa kukutwa ndani ya gesti moja ikisemekana walikuwa na lengo la kuivunjilia mbali amri ya sita ya Mungu.

Binti huyo akidhibitiwa na polisi.Tukio hilo lililojaza umati lilijiri hivi karibuni katika gesti hiyo ambayo inadaiwa haina usajili halali iliyopo jirani na soko. Habari zinasema kuwa, siku hiyo denti wa kike alitumwa sokoni na mama yake kununua mahitaji mbalimbali ya chakula lakini alichelewa kurudi.
 
Ikazidi kudaiwa kuwa mama yake alimfuatilia huku akiwauliza watu, ndipo mbeya mmoja akamtonya kuwa amemwona binti yake akiingia gesti hiyo na kivulana! Mama wa watu, akiwa na mshangao, naye alizama ndani na kuwakuta chumba namba 5. Kikanuka!
Risasi Jumamosi lilifanikiwa kutinga eneo la tukio wakati wa sekeseke hilo na kuzungumza na mashuhuda wawili, Asha Chande na Tausi Omary.Walipohojiwa na mwandishi wetu walisema waliwaona wawili hao wakizama ndani ya gesti hiyo na walishangaa kwa nini walikubaliwa kwa vile wote ni watoto.

...Akizidi kudhibitiwa baada ya kuleta ukorofi.”Baada ya muda mama mmoja mtu mzima alifika hapa 
 
akiwa amefura kwa hasira, akadai binti yake aliyemtuma sokoni ameingia gesti, mara na yeye akaingia ndani, alimkuta yupo na mvulana huyo huku mfuko aliotumwa nao sokoni binti wa kike ukiwa chini ya kitanda.
 
“Aliwafurumusha, kivulana kimekimbia zake na huyu binti ndiyo kama hivi. Mbaya zaidi hapa ni sokoni, watu wameacha biashara na kujaa,” alisema Tausi.
Wakati sakata hilo likiendelea, baadhi ya watu walitaka kumwangushia kipondo denti huyo wa kike kwa kitendo chake cha kuacha alichotumwa na kuzamia kwenye mapenzi akiwa bado mwanafunzi.
Baadaye polisi wa pikipiki walifika na kumchukua denti huyo kwa lengo la kumuokoa na kipigo na kwenda naye Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro ambapo ilidaiwa kuwa polisi walishauri wazazi wa watoto hao wakayamalize nyumbani.

Juhudi za mwanahabari wetu kutaka kuzungumza na mlinzi wa gesti hiyo ziligonga mwamba baada ya muda mwingi kufunga geti kubwa.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya

                                                                    Fasihi simulizi na Andishi HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAIFA NA HULUTISHI . Utangulizi Fasihi simulizi kwa mujibu wa Mlokozi (1996), ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi inafungamana   na muktadha au mazingira fulani ya kijamii na kutawaliwa na muingiliano wa mambo kama vile Fanani, Hadhira, Fani inayotendwa, Tukio, Mahali pamoja na Wakati wa utendaji.             Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake. Mt...