Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Kiswahili

FASIHI LINGANISHI YA KISWAHILI NA TAFSIRI

FASIHI LINGANISHI YA KISWAHILI NA TAFSIRI 1.0 Utangulizi Makala haya yanalenga kufanya uchunguzi katika kazi mbalimbali za fasihi ya Kiswahili zilizotafsiriwa. Katika uchunguzi huu, vitu tutakavyoangalia ni pamoja na mapitio ya fasihi za Kiswahili zilizotafsiriwa, tathimini ya mapitio hayo kwa kuangalia utanzu uliotafsriwa zaidi, lugha zilizojitokeza zaidi katika tafsiri hizo na kisha tutaangalia utanzu unaokabiliwa na changamoto nyingi zaidi wakati wa kutafsiri. Pia tutaangalia uchambuzi wa kazi teule kwa kuangalia kama ni tafsiri   bora au mbovu na kuangalia mchango wa kazi hiyo katika fasihi linganishi ya kiswahili pamoja na chagamoto zitokeazo wakati wa kufasiri matini za kifashi.Na mwisho kabisa ni hitimisho juu ya mjadala huu. 2.0 Usuli Dhana ya Fasihi linganishi kwa kumrejelea Henry Remak (1971) anafasili fasihi linganishi kama uwanja wa kifasihi unaohusika na uchunguzi na mahusianao ya kifasihi nje ya mipaka ya nchi moja, pia kati ya fasihi na fani nyinginezo. K...