Alikuwa ni rita niliyempenda zaidi pale kazini kwetu , kazi yake sikujua ni nini haswa , lakini nilimwona mara kwa mara akipita huku na kule katika shuguli , mimi kazi yangu ilikuwa ni nyingine kabisa . Kampuni yetu ilikuwa kubwa na wafanya kazi wengi , ilikuwa sio rahisi kujua watu wote koz wengine wako idara zingine na shuguli zao ni zingine , ndio kama rita sikujua yeye kazi yake wala yuko idara gani . Lakini alikuwa akipita idara yetu , nikikaa pale katika computer huwa namwona akipita na kuchugulia wakati mwingine anaongea na kiongozi wa idara yetu kisha anaondoka , kweli nilimpenda , siri ilikuwa ni rohoni mwangu . Kwanza nilivutiwa na sauti yake alivyokuwa anaongea upole na taratibu , ngozi yake nyeupe laini sio ya mkorogo , nilivutiwa na macho yake , nywele zake na mwisho kabisa kuliko zote ni miguu yake , vile vimini nilinichanganya kwa hakika . Wakati mwingine nilihisi anakuja kwangu labda kunisalimia hivi au kuniuliza kitu Fulani lakini wapi , hata sal...
Matukio, Habari za Uhakika