Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Ripoti

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI MEI, 2016 UMEONGEZEKA HADI KUFIKIA ASILIMIA 5.2

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa . …………………………………………………………………………   Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2016 umeongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.1 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2016. Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2016 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2016. Kwa mujibu wa wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam, kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Mei, 2016 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula. Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei ni pamoja na mahindi kwa asilimia 1.5, unga wa muhogo kwa asilimia 6.2, nyama ya kuku kwa asilimia 2.6, njegere kwa asilimia 5.8, mihogo mibichi kwa asilimia 8.0 na ndizi za kupika kwa asilimia 2.7. Bi...

Utoro shuleni Bukombe 50% • Kuendekeza ngono, machimbo ya dhahabu vyachangia

MATARAJIO ya wazazi wengi ni kuona watoto wanapoanza shule wanahitimu masomo yao kwa kufikia ngazi za juu za elimu. Hata hivyo, matarajio hayo hayafikiwi katika maeneo mengi hapa nchini kwani watoto wengi hushindwa kuhitimu kutokana na tatizo la utoro.   Tatizo la utoro shuleni ni changamoto kubwa katika sekta ya elimu nchini kwani shule nyingi katika maeneo mbalimbali zinakabiliwa na changamoto hiyo. Miongoni mwa wilaya ambazo tatizo hilo ni kubwa ni pamoja na Wilaya ya Bukombe.   Mkuu wa Wilaya hiyo, Amani Mwenegoha, anasema kuwa utoro katika shule za sekondari kwa wilaya hiyo upo kwa kiwango kikubwa sana kwani takriban nusu ya wanafunzi wote wanaoanza shule mbalimbali wilayani humo huwa hawamalizi masomo yao kutokana na utoro.   Mwenegoha anasema kuwa utoro katika wilaya hii upo kwa asilimia 48 hadi 50 kwa sekondari wakati kwa shule za msingi ni 26%. “Baadhi ya sababu zinachochangia hali hiyo ni kuwapo kwa machimbo ya madini pamoja na baadhi ya wazazi kutok...

Bongo: Dar es Salaam jiji ghali kuishi

Wakazi wa Dar es Salaam hutumia gharama kubwa kufanya manunuzi Wakazi wa jiji la Dar es Salaam hutumia gharama kubwa zaidi, kulipia mahitaji yao ya muhimu kuliko wenzao wengine wa Afrika mashariki, jijini Nairobi na Kampala,utafiti uliofanywa na Shirika linalotathimini gharama za maisha,Numbeo umeeleza. Utafiti huu ulifanywa ukihusisha miji mikubwa 22 ukiangalia uwezo wa kununua bidhaa,biashara za migahawani, hali kadhalika utafiti huu ulijikita kwenye gharama za juu na urahisi wa maisha ya mijini Kwa mujibu wa Ripoti ya Numbeo , takwimu za gharama za watumiaji kwa wakazi wa Dar es Salaam kwenye bidhaa na huduma mbalimbali ni asilimia 62.83 ambayo imezidi Kampala na Nairobi zenye asilimia 54.34. Kwa sasa Kenya ni nchi inayoongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa Afrika Mashariki na iko nafasi ya sita barani Afrika, hata hivyo kwa mujibu wa matazamio ya Benki ya Standard Charterd , Tanzania inaelekea kuipiku Kenya na kuwa nchi yenye uchumi mkubwa ifikapo mwaka 2030 iwapo pato la t...

Idara ya polisi yaongoza kwa ufisadi TZ

Jeshi la polisi nchini Tanzania ndio taasisi fisadi zaidi chini  Idara ya polisi ndio taasisi inayochukua hongo zaidi nchini Tanzania kulingana na ripoti ya ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki. Ripoti hiyo inasema kuwa maafisa wa polisi walipokea asilimia 25 ya hongo zote zilizotolewa kwa wafanyikazi wa taasisi za uma mwaka uliopita. Ya pili ni idara ya mahakama,ambayo wafanyikazi wake walitia mfukoni asilimia 18 ya hongo,huku mashirika yalio na majukumu ya usajili na utoaji wa leseni yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia 10. kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Idara ya Polisi nchini Tanzania imetajwa kuwa ya tatu kwa ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki. Polisi wa Uganda wanaongoza wakifuatiwa na wale wa Kenya katika nafasi ya pili na wale wa Burundi wakiwa katika nafasi ya nne. Kulingana na ripoti hiyo maafisa wa polisi wa Rwanda ndio wasiochukua hongo ya juu Afrika mashariki. Utafiti huo ulifanywa mwezi Julai na Ago...

Ripoti: Tanzania kinara wa utumwa A.Mashariki

Ri poti mpya ya kimataifa kuhusu hali ya utumwa duniani imeitajaTanzania kuongoza Afrika Mashariki. Dar es Salaam. Ripoti mpya ya kimataifa kuhusu hali ya utumwa duniani imeitajaTanzania kuongoza Afrika Mashariki kwa kuwa na zaidi ya watu 350,000 wanaotumikishwa maeneo mbalimbali nchini. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, jana alikiri kuwapo kwa tatizo hilo akisema: “Ni kweli kuwa wafanyakazi wa ndani wanatumikishwa hapa nchini ikilinganishwa na nchi nyingine.” Ripoti hiyo ijulikanayo kama ‘The Global Slavery Index 2014’, iliyotolewa nchini Australia Novemba mwaka huu, inaonyesha kuwa Tanzania inashika nafasi ya 14 barani Afrika na kuwa ya 33 duniani. Imeitaja Uganda kuwa ndiyo inayoshika nafasi ya pili kwa kuwa na watumwa 135,000, ikifuatiwa na Rwanda (83,600), Burundi (72,300) huku Kenya ikiwa na watumwa 64,900. Utafiti huo uliofanyika katika nchi 167 duniani, unatafsiri utumwa kuwa ni hali ya mtu kumhifadhi mtu mwingine na kumnyima u...