Skip to main content

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI MEI, 2016 UMEONGEZEKA HADI KUFIKIA ASILIMIA 5.2

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa .
…………………………………………………………………………
 
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2016 umeongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.1 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2016.

Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2016 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2016.

Kwa mujibu wa wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam, kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Mei, 2016 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei ni pamoja na mahindi kwa asilimia 1.5, unga wa muhogo kwa asilimia 6.2, nyama ya kuku kwa asilimia 2.6, njegere kwa asilimia 5.8, mihogo mibichi kwa asilimia 8.0 na ndizi za kupika kwa asilimia 2.7.

Bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 2.9, mkaa kwa asilimia 2.5, dizeli kwa asilimia 4.6, petroli kwa asilimia 2.5 na vifaa vya michezo kwa asilimia 7.8.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Mei, 2016 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umebaki kuwa asilimia 0.5 kama ilivyokuwa mwezi Aprili, 2016. Aidha, Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 103.00 mwezi Mei, 2016 kutoka 102.46 mwezi Aprili, 2016.

Aidha, ulinganifu wa Mfumuko wa Bei kwa baadhi ya  nchi  za Jumuia ya Afrika Mashariki, taarifa hiyo inaonyesha kuwa Mfumuko wa Bei nchini Uganda kwa mwezi Mei, 2016 umeongezeka hadi kufikia  asilimia 5.4 kutoka asilimia 5.1 kwa mwezi Aprili, 2016.

Kwa upande wa Kenya, Mfumuko wa Bei umepungua hadi kufikia asilimia  5.00 kwa mwezi  Mei, 2016 kutoka asilimia 5.27 iliyorekodiwa mwezi Aprili, 2016.
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya

                                                                    Fasihi simulizi na Andishi HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAIFA NA HULUTISHI . Utangulizi Fasihi simulizi kwa mujibu wa Mlokozi (1996), ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi inafungamana   na muktadha au mazingira fulani ya kijamii na kutawaliwa na muingiliano wa mambo kama vile Fanani, Hadhira, Fani inayotendwa, Tukio, Mahali pamoja na Wakati wa utendaji.             Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake. Mt...