Skip to main content

STAA WA FILAMU BONGO.RAY AMSALITI CHUCHU KWA HUSNA, WANASWA USIKU


MUIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, amedaiwa kumsaliti mpenzi wake wa siku nyingi, Chuchu Hans baada ya kukutwa akiwa amepozi kimahaba na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011, Husna Maulid katika Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar, hivi karibuni.



 Muigizaji nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ akipozi kimahaba na Husna Maulid.
Wawili hao waliokuwa wamepakatana, walikutwa katika ukumbi huo wakati bendi mbili kubwa za muziki wa dansi nchini, FM Academia na The African Stars ‘Twanga Pepeta’ zilipokuwa zikiangusha burudani kabambe ya kushindana.
Uwepo wa Ray na Husna ulitafsiriwa kuwa ni usaliti kwani muda wote waliokuwa ndani ya ukumbi huo wawili hao walikuwa wamegandana kimahaba huku wataalamu wa ubuyu wakikazia madai kwa kusema wawili hao ni wapenzi.
 
 
Husna Maulid akisisitiza jambo kwa Ray.
“Sasa wewe kusoma hujui hata picha huoni? Hawa watakuwa ni wapenzi tu, haiwezekani mtu mpakatane, mpeane kampani kiasi hiki na mtu ambaye siyo mtu wako,” alisikika shuhuda mmoja.
Ray ambaye kabla ya kuwa na Chuchu aliwahi kutoka kimapenzi na mwigizaji Blandina Changula ‘Johari’ na Ruth Suka ‘Mainda’, alionekana kufurahia kumpakata Husna huku wakipeana kampani ya kuzungumza, lakini alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa akifuatiliwa na kamera ya paparazi wetu.
Kutokana na mazingira ya wawili hao ukumbini hapo, paparazi wetu alishindwa kuzungumza nao juu ya ishu hiyo na hata alipowatafuta kwa simu siku iliyofuata, simu zao ziliita bila kupokelewa (huenda walijua wataulizwa nini).Lakini Chuchu, ambaye ndiye ‘mmiliki’ wa Ray hivi sasa, alipoulizwa kama anajua lolote juu ya ukaribu wa watu hao, alishtuka na kudai haamini kama Ray anaweza kumsaliti au amewahi kupiga picha na Husna za kimahaba.
 
Muigizaji nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray.
“Khaa! Unasemaje? Mimi siamini labda kama kuna picha zao za pamoja naomba unitumie Whatsapp nizione maana nashindwa niongee nini, sikujua kama walienda popote Ray na Husna.”
Mwanahabari wetu alimtumia picha hizo Chuchu lakini hadi tunakwenda mitamboni, mrembo huyo hakuwa amejibu kitu chochote.
 
Chanzo global Publishers

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya

                                                                    Fasihi simulizi na Andishi HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAIFA NA HULUTISHI . Utangulizi Fasihi simulizi kwa mujibu wa Mlokozi (1996), ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi inafungamana   na muktadha au mazingira fulani ya kijamii na kutawaliwa na muingiliano wa mambo kama vile Fanani, Hadhira, Fani inayotendwa, Tukio, Mahali pamoja na Wakati wa utendaji.             Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake. Mt...