Skip to main content

DALILI TANO MBAYA KWENYE UHUSIANO UKIONA, UJUE MPENZIO ANACHEPUKA


Leo naomba pia niongelee kuhusu dalili ambazo zinaweza onekana kwa mwenza wako ambazo zinapelekea kujenga fikra kwamba  "unasalitiwa" dalili hizo ni kama zifuatazo:-

1.Nakupenda lakini Sina Hisia nawe(Kwa wale ambao bado hawajaoana)
Hii ni dalili kwamba Mpenzi wako ana mtu mwingine nje na inawezekana kabisa kwamba yeye ndo anapendwa zaidi yako wewe hata kama muda mwingi upo nae! Anakutumia tu huyo ! 

2.Sisi ni Marafiki tu!
Kwa ambao bado hawajaoana Ukimuuliza Mpenzio unanichukuliaje au mimi ni nani kwako anakuwa anasuasua sana sana utaambiwa ni marafiki tu.Na kwa ambao tupo katika Ndoa ukiuuliza vipi mbona nakuona una mazoea ya karibu mno na mtu fulani? Utaambiwa ni Rafiki tu! 

3 Nahitaji muda wa kufikiria kuhusu hisia zangu!
Hili nijibu tosha kwamba Kuna Mwenzio ambaye anamchanganya akili mpenzi wako na ndio maana anakuwa hivyo! Anza kukaa tayari au mguu nje, mguu ndani!

4.Mabadiliko ya Ratiba za Kazi
Kwa wale ambao tupo ndani ya ndoa au mahusiano ya muda mrefu, utaliona hili, mara kurudi late sana, ubize umekuwa mwingi mno hadi weekend! Na dharula za kikazi zisizoisha mara vikao mara n.k !

5. Kutumia Muda Mwingi katika Computer
Kama ameweza kujizuia kutoka toka hovyo, basi anaweza kuwa mtumiaji mzuri na wa muda mrefu wa Computer, atakaa hapo ata chat na kuongea na wezi wako tani yake, na unaweza usilijue hili kwani atakuambia ana kazi za ofisini anamalizia!

6. Simu za Siri, Simu kuwa locked !
Siku hizi simu zimekuwa nyingi, za usiku, mara simu ikipigwa ananyanyuka kwenda chumbani au kujificha kidogo, mara simu ikipigwa inakwatwa au inawekwa silent ! Pia mambo ya kulock simu na hizi SmartPhone sasa mtu akishatupia kitu cha Pattern/Password/PIN ndo basi tena unatakiwa kuwa mjanja sana kuweza kumkamata.! 

7. Tabia yoyote yenye kutia Mashaka!
Waswazi wanasema "Wasiwasi ndo Akili" Basi wasiwasi wako huenda ukakupa akili juu ya nini kinachoendelea na ukapata njia ya kuubaini ukweli! 
Ukiyaona haya au ya kufanana na haya kaa ukijua kuna kidudumtu kinawala na kitawatenganisha, Ni vyema ukachukua hatua! Pia Jiandae Kudanganywa! As some people says kuwa love is a game so get ready kuplay na sio kuplay na kuwa loser but to be a winner.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya

                                                                    Fasihi simulizi na Andishi HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAIFA NA HULUTISHI . Utangulizi Fasihi simulizi kwa mujibu wa Mlokozi (1996), ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi inafungamana   na muktadha au mazingira fulani ya kijamii na kutawaliwa na muingiliano wa mambo kama vile Fanani, Hadhira, Fani inayotendwa, Tukio, Mahali pamoja na Wakati wa utendaji.             Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake. Mt...