Aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Nyerere ameingia kwenye list ya wagombea ubunge mwaka 2015
Kwenye interview na millardayo.com Steve amesema ‘Kwanza
ninataka kuwahakikishia watanzania sijakurupuka, nimekuwa mwanachama
wa chama cha Mapinduzi umoja wa vijana almost miaka 25 na sasa hivi
nina miaka 29 naelekea 30 lakini vilevile nimekuwa kamanda wa vijana
miaka 10 tawi la bwani kinondoni, nimekuwa muhamasishaji wa chama cha
mapinduzi kitaifa kwa muda wa miaka 10′
‘Sijakurupuka
na wala sijatamkia sifa kwasababu labda nimeona mtu fulani amegombea,
kinondoni kuna matatizo kadhaa nani anaweza kuyatetea hayo matatizo?
nitakuwa mtetezi pamoja na matatizo ya wasanii wetu, kuhusu kazi zangu
za filamu nitakuwa nafanya kama kawaida huku nikiwa natumikia kazi za
Bungeni’
ATAACHA KUIGIZA?!
Amejibu
>>> ‘Kazi yangu ya sanaa sitoweza kuiacha nadhani naweza kuwa
ndio Mbunge wa kwanza yuko ndani ya Bunge na bado yuko kwenye sanaa
anacheza filamu’
Unaweza ukasikiliza alichokizungumza Steve Nyerere kwa kubonyeza play hapa chini
Comments
Post a Comment