Dk. Harrison Mwakyembe |
July 21 2016 Waziri wa katiba na sheria, Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds 360 cha clouds TV na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu katiba na sheria na hili sakata la Richmond likagusiwa.
Mtangazaji wa clouds TV, Hudson Kamoga alimuuliza Waziri mwakyembe kuhusiana na sakata la Richmond wakati akiwa mwenyekiti wa kamati iliyokuwa inachunguza sakata hilo ambapo walikuja na ripoti ambayo ilipelekea aliyekuwa Waziri mkuu kwa wakati huo, Edward Lowassa kujiuzulu. Hudson ametaka kujua kama kuna mambo ambayo watanzania hawakuyajua kuhusu sakata la Richmond
Waziri Mwakyembe amesema ….>>>‘kesi ya Richmond tuliifanya kwa roho safi na kwa kupiga magoti kwa Mungu na tuliifanya haki kwa kila mtu tulichoamua hata tuamue kesho asubuhi nirudie tena hata koma haitabadilika itakuwa vilevile na mimi nitafurahi sana’
>>>’chini ya kanuni tunaruhusiwa kuifufua tena Richmond ili ichunguzwe upya na ninaaapa wanaweza wote wakahama wakaniacha peke yangu na uhakika mimi mwenyewe nilichonacho nitajenga hoja sidhani kama kuna mtu hata mmoja atasalimika kwenda jela‘