Matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne Yatangazwa....... St. Franscis, Kilimanjaro Islamic na Kaizerege Zaongoza
Baraza la Mitihani nchini – NECTA limetoa matokeo ya mitihani ya upimaji kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa shule zote za msingi nchini pamoja na ule wa kidato cha pili kwa wanafunzi wa shule za sekondari yanayoonesha ufaulu kuongezeka kwa 1.9%. Katibu Mtendaji wa Baraza lza Mitihani nchini Dkt Charles Msonde ndiye aliyetoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo katika hali isiyo ya kawaida, shule tisa kati ya kumi zilizofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha pili nchini, zimetoka mkoani Mtwara kama zinavyoonekana hapa Amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.9 kutoka 89.12% mwaka 2015 hadi kufikia 91.02% mwaka 2016 ambapo wanafunzi 372,228 wamepata alama zinazowawezesha kuingia kidato cha tatu huku wanafunzi 36,737 wakishindwa kufikisha alama hizo. Shule ya St. Francis Girls ya Mbeya imeongoza katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016 Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya I, II, na ...