Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2017

Soma Magazeti ya Tanzania April 14, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU WA MASOMO YA HISABATI NA SAYANSI KWA MWAKA 2016/2017

Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017. Majina ya Walimu yaliyotangazwa yanatokana na tangazo la nafasi ya kazi ya Ualimu lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mnamo tarehe 01 Desemba, 2016. Jumla ya Walimu wapya wapatao 3,081 wakiwemo 1,544 ni wa ngazi ya Shahada na Walimu 1,537 ni wa Stashahada. Walimu hao watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi tarehe 25 Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI), vyeti halisi vya kitaalaam vya kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Shahada na Cheti cha kuzaliwa. Angalizo : i. Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi waliohitimu hadi mwaka 2014/2015. ii. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio m...

AJIRA MPYA ZA WALIMU WA HISABATI NA SAYANSI 2016/2017

Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017. Orodha ya Walimu wa Shahada wa Ajira Mpya kwa Masomo ya Sayansi na Hisabati. Orodha ya Walimu wa Ajira Mpya kwa Masomo ya Sayansi na Hisabati.

Breaking News: Msani Roma Mkatoliki na wenzake waliotekwa wapatikana Wakiwa Salama

Muda mfupi  baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro kuwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kusema ni lini mwanamuziki  Roma na wenzake watapatikana, taarifa kutoka kwa mmiliki wa studio walipokamatiwa, amethibitisha kuwa wamepatikana. J Murder ambaye ndiye mmiliki wa Tongwe Records walipokuwa Roma na wenzake kabla ya kukamatwa na watu wasiojulikana, amesema kuwa wasanii hao wamepatikana na wapo katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Aidha,Mkuu wa polisi (OCD) wilaya ya Kinondoni, Abubakar Kunga amethibitisha kupatikana kwa wasanii hao, lakini kwa sasa amesema wanafanya nao mahojiano ya kipolisi katika kituo cha Oysterbay. Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru. Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii...

Taarifa Toka IKULU: Rais Magufuli Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa EU, Roeland Van de Geer na Balozi wa Israel, Yahel Vilan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Aprili, 2017 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Geer na kuushukuru umoja wa nchi hizo kwa kutoa msaada wa Euro Milioni 205 sawa na takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo hapa nchini kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia mwaka huu. Mhe. Rais Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo kumethibitisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na kwamba pamoja na kutoa fedha hizo umoja huo unatarajia kutoa fedha nyingine kiasi cha Euro Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendeleza viwanda, kilimo na uzalishaji wa nishati. “Nimefurahi sana kwamba uhusiano na ushirikiano wetu unajikita kushughulikia mambo ya msingi kwa Watanzania, nakuhakikishia kuwa fedha mnazotoa zitatumika vizuri na zitatoa mchango mkubwa katika maendeleo yetu” amesema Mhe. Dkt. Magufuli. Nae Mhe. Balozi Roeland Van de Geer amempon...