Stori: Chande Abdallah na Haruni Sanchawa/Uwazi
DUNIA imekwisha! Binti mmoja mwenye umri wa miaka 19, Rukia Ally anadaiwa kumuua kwa kumchoma kisu kaka yake wa kuzaliwa, Said Ally wote wakati whga Tegeta Mivumoni, Kata ya Wazo jijini Dar es Salaam, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana na kijana huyo kutaka kudhibiti tabia zisizofaa za dada yake huyo, tukio lililotokea usiku wa Januari 24 mwaka huu.
Rukia Ally anayedaiwa kumuua kwa kumchoma kisu kaka yake, Said Ally.
Kwa mujibu wa habari kutoka eneo la tukio, inadaiwa kuwa binti huyo alikuwa na kawaida ya kuondoka nyumbani kwao na kwenda kusikojulikana ambako wakati mwingine alikuwa akikaa zaidi ya siku tatu pasipo kurejea nyumbani, huku akiwa hana maelezo ya kutosha.
Inadaiwa kuwa siku hiyo, msichana huyo hakuwa amerudi nyumbani kwa siku tatu, hivyo aliporejea saa tatu usiku, kaka yake alimuuliza alikokuwa, lakini badala ya kumjibu, alimuomba aingie kwanza ndani kwake na kuwa atarejea ili kumpatia majibu.
Mama wa marehemu Fatuma (katikati) akifarijiwa kwa kumpoteza mwanaye
Aliporejea na kuulizwa swali hilo na kushindwa kutoa majibu ya kueleweka, kaka huyo alimchapa na fimbo mguuni kama ishara ya kumkanya, lakini inadaiwa Rukia alichomoa kisu alichokuwa amekificha nguoni mwake na kumchoma nacho upande wa kushoto wa kifua chake.
Mama wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma, alisema binti yake alikuwa na tabia zilizowakwaza ndugu zake, kama kuvaa nguo fupi na kuondoka nyumbani bila kuaga.
Waombolezaji wakiwa msibani.
“Kwa sababu mdogo mtu hakuwa msikivu kwa kaka yake, ndipo kaka mtu akachukua bakora na kumchapa nayo mguuni kwa lengo la kumkanya, ndipo ghafla nikashangaa kumuona Rukia akimchoma kisu kaka yake kifuani na kukichomoa kisha akakimbia na kukitupa kwenye majani.
“Kauli aliyoitoa kaka yake ni kwamba: Mdogo wangu unaniua! Akadondoka hapohapo, nikamkimbilia na kumpakata miguuni mwangu damu zikimtoka mpaka anakata roho nilikuwa nikimtazama,” alisema mama huyo.
Kisu kilichotumiwa kwa mauaji.
Aidha shangazi wa marehemu, Mariam Saidi alidai baada ya Rukia kukimbia, alizungumza naye kwa simu lakini baadaye hakupatikana tena.“Alinipigia nikaongea naye, akasema nimwambie mama yake awadanganye polisi kuwa yeye hakumuua kaka yake, bali alivamiwa na majambazi, nilipomuuliza yupo wapi nikamchukue alisema yupo Ubungo halafu hakupatikana tena,” alisema Mariam.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha alisema binti huyo alikuwa na tabia ya kutembea usiku na kuvaa nguo fupi kwani kuna siku alikutana naye usiku wa manane akiwa na rafiki yake wakitokea kwenye klabu moja ya usiku.
Marehemu Said Ally enzi za uhai wake.
Taarifa zilizoifikia gazeti hili kutoka kwa mwenyekiti huyo zilidai kuwa Rukia alikamatwa Mkuranga jioni ya Januari 24 akiwa anaelekea mafichoni na amefikishwa kituo cha polisi Wazo Hill kwa ajili ya hatua za kisheria huku mazishi yakifanyika siku hiyo hiyo.
Comments
Post a Comment