Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemsifu mshambuliaji wake Ddier Drogba kwa kusema kuwa bado kuna mengi ya kutegemewa toka kwa mchezaji huyo na hajaisha kama inavyodhaniwa na wengi .
Mourinho alisema hayo kwenye hafla maalum ya utoaji wa tuzo ya heshima kwa Dorgba ambayo iliandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo nchini England .
Hafla hiyo iliyoandaliwa na waandishi ililenga kumtunukia tuzo ya heshima mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast kwa mchango wake kwenye mchezo wa soka na kwenye ligi ya England kwa jumla
Drogba hapo jana alipewa tuzo ya heshima na chama cha waandishi wa habari za michezo England .
Mourinho alimsifu Dorgba akimuita mchezaji mwenye thamani ya kipekee kwa timu hiyo baada ya mchango wake kuipa mafanikio mbalimbali tangu alipojiunga nayo mwaka 2004 wakati aliposajiliwa toka Olympique Marseile .
Tuzo kama hii imewahi kutolewa kwa kocha Jose Mourinho na Sir Alex Fergusson pamoja na wachezaji kama David Beckham baada ya mafanikio ya muda mrefu .
Akiwa Chelsea Drogba ametwaa zaidi ya mataji 10 likiwemo taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2012.
Drogba mwenyewe kwa upande wake aliishukuru klabu ya Chelsea kwa kumpa nafasi ya kupata mafanikio ambayo labda asingeyapata kwenye klabu nyingine na akasisitiza kuwa ataendelea kuwa sehemu ya familia ya Chelsea kwa muda mrefu ujao .
Mourinho alimsajii Drogba mwaka 2004 wakati mshambuliaji huyo akitokea Olympique Marseile.
Mourinho ameonyesha dhamira ya kutaka kuendelea kuwa na mchezaji huyo kwa ajili ya msimu ujao baada ya kusema kuwa kuna mengi ya kutarajiwa toka kwa Drogba na watu hawapaswi kudhani kuwa ameisha na anangoja kustaafu .
Comments
Post a Comment