Kocha wa klabu ya Juventus Masimiliano Allegri amechochea tetesi za kuondoka kwa nyota wake Paul Pogba baada ya kuwataka mashabiki wa klabu hiyo kumtazama Pogba kwa kipindi hiki wakati akiwa Juventus kwani huenda wasipate nafasi hiyo tena .
Pogba mwishoni mwa wiki iliyopita alifunga bao moja huku akisaidia kutengeneza bao jingine katika mechi ya Juventus dhidi ya Chievo Veron amechi ambayo Juve walishinda 2-0 ukiwa muendelezo wa kiwango bora ambacho ameendelea kukionyesha tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Manchester United .
Tetesi mbalimbali zimemhusisha Pogba na kujiunga na klabu kadhaa barani ulaya zikiwemo Paris St Germain , Real Madrid , Manchester City , Chelsea na Manchester United ambazo kwa nyakati tofauti zimehusishwa na nyota huyo .
Pogba mwenyewe ameonekana kuziongeza kasi tetesi hizi baada ya kusema kuwa angependa kurudi Manchester United huku kwa wakati mwingine akisema kuwa ameanza kujifu nza lugha ya kihispania ambapo kauli hiyo imehusishwa na mpango wa kujiunga na mabingwa wa ulaya .
Paul Pogba amekuwa akizungusha vichwa vya makocha mbalimbali wa timu kubwa barani ulaya kwa kiwango alichoonyesha akiwa na Juventus . |
Juventus tayari wanaonekana kujiandaa kumpoteza nyota huyu baada ya kocha wa timu hiyo kusema kuwa hakuna kinachomzuia mchezaji hasa kama anapatikana kwa bei itakyoleta faida kwa klabu . Juventus wameweka bei ya paundi jmilioni 77 kwa ajili ya nyota huyu toka kwa timu yoyote itakayotaka kumsajili ambapo Juventus itatumia fedha hizi kusajili nyota wengine watatu au wanne ili kujiimarisha zaidi
Comments
Post a Comment