Skip to main content

WANASWA WAKIFANYA MAPENZI KITUO CHA POLISI


AMA kweli binadamu siyo waoga! Watu wawili ambao majina yao hayakupatikana mara moja, waliamua kujitoa fahamu na kuamua kufanya mapenzi ndani ya gari nje ya Kituo cha Polisi cha Alimaua kilichopo Kata ya Kijitonyama jijini Dar, OFM wanakumegea mkanda mzima.
Watu hao wakiendelea kufanya mambo yao.
Tukio hilo la aina yake lilinaswa saa nane usiku wa Jumatano wakati kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kikiwa kazini kusaka matukio mbalimbali ya usiku mnene.
Ilikuwaje?
Awali, baadhi ya watu waliokuwa wakitoka kuangalia mechi ya Kombe la Capital One kati ya Chelsea na Liverpool nchini Uingereza waliwaona wawili hao wakipaki gari eneo hilo la polisi kana kwamba walikuwa na shida muhimu ya kiusalama kama si kisheria. Kituo hicho kilikuwa kimefungwa!
Tofauti na matarajio ya mashuhuda hao, gari hilo aina ya Toyota Mark II (namba za usajili tunazo) lilizimwa taa za ndani na kuachwa ikiunguruma kisha watu hao ambao haikufahamika kama ni wapenzi au ni changudoa na mteja wake walianza kushikana kimahaba.
DEREVA ALALIA USUKANI
OFM walizidi kuambiwa kuwa, mashuhuda walijiongeza na kubaini kwamba wawili hao walikodi gari hilo kwani walipoanza kushikana, dereva aliegemea usukani kwa hali iliyotafsirika kuwa, alikuwa akiwapa nafasi abiria wake wamalize ‘mambo’ yao.
He! Mchezo wAnoga
Muonekano wa kituo hicho.
“Unaweza kusema wawili hao walikuwa ndani ya fensi nyumbani kwao, kwani wanazidi kufanyiana mambo ya chumbani. Hivi hapa sisi tunawashangaa,” shuhuda mmoja aliwaambia OFM.
OFM WATINGA
Ndani ya dakika chache, makamanda wa OFM wanaopatikana kwa saa 24, walikuwa wamewasili eneo la tukio kwa kutumia pikipiki zao maalum ziendazo kasi.
Kitendo bila kuchelewa, zoezi la kuwafotoa picha kwa mbali lilianza na ndipo waliposhituliwa na mwanga wa ‘flash’, hali iliyomfanya dereva wa gari hilo kutaka kuondoa gari.
WATAITIWA, WAKUTWA CHAKARI
Kwa kutumia ujasiri wa hali ya juu, makamanda hao kwa kusaidiana na mmoja wa mashuhuda anayeishi eneo hilo walilizuia gari lisiondoke na ndipo ilipobainika kuwa, licha ya kunaswa wakiibanjua amri ya sita ya Muumba pia watu hao walikuwa chakari kwa pombe.
WASHINDWA KUJIBU MASWALI
Hata hivyo, kutokana na kuwa tilalila, ilikuwa vigumu kuwahoji kwani kila walipoulizwa kwa nini waliamua ‘kupumzikia’ nje ya kituo hicho cha polisi, waliishia kuinamisha vichwa.
OFM YAMTOA NDUKI DEREVA
Mazingira hayo yaliwalazimu makamanda wa OFM kumwamuru dereva ambaye alikuwa akijitambua kuliondoa gari hilo kituoni hapo kabla msala mkubwa haujawapata.
Zote hizo pombe
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura.
Uchunguzi uliofanywa na OFM umebaini kuwa, kitendo cha watu hao kupaki gari eneo la kituo cha polisi na kufanya uzinzi kilitokana na pombe walizokuwa wamekunywa hivyo akili yao iliwatuma kuwa lile lilikuwa eneo salama zaidi kwao.
OFM WAMSAKA KAMANDA WA POLISI
Ili kutaka kujua ni kwa nini kituo hicho cha polisi kilipigwa ‘loki’ wakati usiku ndiyo matukio ya uhalifu yako kwa wingi, OFM walimwendea hewani Kamanda wa Polisi     Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura.
OFM: “Afande, habari?”
Wambura: “Nzuri.”
OFM: “Naongea na RPC wa Kinondoni?”
Wambura: “Unasemaje?”
OFM: “Mimi ni mwandishi napiga simu kutoka Global Publishers...”
Wambura: “Nipo kwenye mkutano. Nenda ofisini (Oysterbay Polisi) utamkuta mhusika.”
OFM: “Naomba unisaidie pale nitamkuta nani? Au namba yake ya simu.”
Wambura: “Ifike mahali sasa, waandishi muwe mnafika ofisini kwa taarifa kama hizi (za kiofisi). Nitajuaje kama wewe ni mwandishi? Nenda pale utaoneshwa kaimu kamanda uzungumze naye.”
OFM OYSTERBAY POLISI
OFM walifunga safari hadi Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar na kumuulizia kaimu kamanda wa mkoa lakini afande aliyekuwa mapokezi alisema ametoka kikazi nje ya kituo.

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

REALD MADRID YATOKA SARE NA VALENCIA,RONALDO AKOSA PENATI>> Angalia hapa

Cristiano Ronaldo's face tells the story as Real Madrid fail to beat Valencia and leave themselves a near impossible task to catch Barcelona Valencia forward Paco Alcacer celebrates scoring the 19th-minute opener for the underdogs against Real Madrid  Valencia players celebrate their second goal after Javi Fuego heads beyond Iker Casillas from a free-kick Valencia form a huddle as they regroup after taking a 2-0 lead against the side pushing to catch Barcelona in La Liga Ronaldo holds his head in his hand after Real concede their second goal of the match on Saturday evening at the Bernabeu Real Madrid's Javier Hernandez (right) shows his disbelief after missing a golden opportunity to score German midfielder Toni Kroos (right) is upended by Valencia midfielder Andre Gomes during a physical first half Ronaldo signals as Real prepare to restart play after conceded the second goal of the match  Ronaldo steps up for the penalty and a chance to peg one back for his side at 2-0 do...