Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2015

Download Diamond Platnumz Ft. P-Square

Sikiliza nyimbo mpya ya Diamond ft P-Square hapa

Waliowajeruhi polisi TZ wasakwa

Polisi nchini Tanzania  Polisi nchini Tanzania wamesema wanawasaka watuhumiwa waliowajeruhi askari sita kwa risasi mkoani Tanga. Askari hao walijeruhiwa wakati wakifanya kazi ya kuwatafuta watuhumiwa wa uhalifu wa kutumia silaha wanaodaiwa kuwa walijificha eneo moja nje ya mji wa Tanga wakiwa na silaha. Awali kulizagaa taarifa na hofu kuwa wahusika walikuwa na itikadi za kigaidi, lakini taarifa ya maandishi iliyotolewa na polisi imewaita watu hao kuwa ni majambazi na kwamba msako wa kuwatafuta unaendelea. Hata hivyo taarifa haikuleleza wanaotafutwa ni watu wangapi, ingawa imetaja kuhusika kwa jeshi lenye silaha jambo linaloashiria mapambano yalikuwa makal

Zuma: hakuna ruhusa mgeni kumiliki ardhi

Wageni hawatoruhusiwa kumiliki ardhi Afrika Kusini, kufuatana na sheria kali zinazopendekezwa na Rais Jacob Zuma. Siku zijazo wageni wataruhusiwa tu kukodi kwa muda mrefu ardhi ya mashamba ya Afrika Kusini. Mbali ya hayo, mtu yeyote anayemiliki zaidi ya hekta 12,000 atalazimishwa kuiuzia serikali ili ipate kugawiwa. Ardhi bado ni swala linalozusha hamasa nchini humo - ambako karne tatu za ukoloni na ubaguzi wa rangi - zimeacha ardhi nyingi mikononi mwa wachache, hasa wazungu. Tangu kumalizika ubaguzi wa rangi mwaka 1994, chama tawala cha ANC, kimeshindwa kufikia lengo lake la kugawa thuluthi ya ardhi ya kilimo kwa Waafrika, ulipofika mwaka 2014.

Soma hapa kurasa za mwanzo na mwisho za Magazeti ya leo February 15, 2015

  . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA CHA SITA KWA KUTUMIA MFUMO WA GPA

CHRISTIAN BELLA AACHA HISTORIA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE

Christian Bella akiimba na mashabiki wimbo wa Usilie. Bella akiwakonga mashabiki jukwaani. Bella akimpa maiki mmoja wa kinamama waliojitokeza jukwaani kuimba Wimbo wa Nani Kama Mama. Wanenguaji wa Malaika Music wakifanya yao jukwaani. Baadhi ya mashabiki wakijiachia kwa kucheza Wimbo wa Nakuhitaji wa Christian Bella. Umati wa mashabiki wakimfuatilia Bella (hayupo pichani) alipokuwa akiimba Wimbo wa Usilie. MFALME wa masauti 'Christian Bella' akiwa na bendi yake ya Malaika Music wameandika historia mpya ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala. Bella alianza kwa kuimba nyimbo zake kali za mapenzi kama vile Msaliti, Usilie, Nakuhitaji sambamba na kutambulisha wimbo wake mpya wa Nashindwa. Burudani ilinoga zaidi pale alipomaliza kwa Wimbo wa Nani Kama Mama huku akiimba pamoja na wakinamama wote waliojumuika naye jukwaani.

MZEE YUSUF AFUNIKA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE

Mfalme Mzee Yusuf akiimba na mashabiki wimbo wake mpya wa Mahaba Niue. Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa My Valentine. Muimbaji wa Jahazi, Leila akiimba Wimbo wa Fanya Yako. Khadija Yusuf naye akiimba na mashabiki wimbo wake wa Hasidi Hana Sababu. Mwansiti Mbwana akiwakonga na Wimbo wa Alipangalo Jalali. Waimbaji wa Jahazi wakiwa katika picha ya pamoja. Mashabiki wakimzunguka bi'dada (jina lake halikujulikana) akiyakata mauno. Umati wa mashabiki wakipagawa na Jahazi Modern Taarab. KUNDI linalotikisa kunako miondoko ya Pwani, Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf leo limefunika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live katika shoo maalum ya Usiku wa Wapendanao 'Valentine's Day'. Jahazi walianza kutawala jukwaa ambapo, Leila alikuwa wa kwanza kupanda na kuimba Wimbo wa Fanya Yako kisha akafuatiwa na Mwansiti na Fatuma Nyoro. Baadaye alipanda Mzee Yusuf kwa Wimbo wa My Valentine na kufanya ukumbi wote kulipuka kwa shangwe. Mzee Yusuf ali...