MFALME wa masauti 'Christian Bella' akiwa na bendi yake ya Malaika Music wameandika historia mpya ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala.
Bella alianza kwa kuimba nyimbo zake kali za mapenzi kama vile Msaliti, Usilie, Nakuhitaji sambamba na kutambulisha wimbo wake mpya wa Nashindwa. Burudani ilinoga zaidi pale alipomaliza kwa Wimbo wa Nani Kama Mama huku akiimba pamoja na wakinamama wote waliojumuika naye jukwaani.
Comments
Post a Comment