Skip to main content

MVUA YAGEUKA KERO KUBWA KWA WAKAZI WA DAR


Soko la Mchikichini, Ilala-Boma linavyoonekana kufuatia mvua za sasa
Maji yalivyotapakaa soka la Sinza Afrika-Sana.
Wakazi wa Mwanayamala-Mkwajuni wakitoa maji katika nyumba zao.
...Juhudi za kuondoa maji zikiendelea.

Mwonekano wa nyumba za bonde la Mchikichini, Ilala-Boma.
WAKATI mvua zikiendela kunyesha katika jiji la Dar es Salaam, na sehemu nyingine nchini, wakazi wake wengi wameonekana kuhangaika kupata sehemu salama za kuishi na kufanyia biashara.Mtandao huu umezungukia maeneo mbalimbali ya jiji na kukuta wakazi wa maeneo mengi wakitoa maji kwenye nyumba zao na sehemu za kufanyia biashara.
 
Wakiongea na mwandishi wetu, wakazi wa maeneo ya Mwanayamala-Mkwajuni maarufu kama Bondeni, wameitupia lawama kampuni ya ujenzi ya Strabag kuwa imechangia nyumba zao kuingiliwa na maji kwani mifereji iliyotengenezwa haikidhi uwezo wa kusafirisha maji kwa kasi kwani ni midogo na badala yake maji hujaa na kuelekea katika makazi yao.
 
Katika maeneo ya Jangwani mtandao huu ulikuta baadhi ya nyumba zilizoko bondeni zikiwa karibu kumezwa na maji, ambapo wakazi wa maeneo hayo wametaka serikali iwasaidie.
Katika soko la Sinza Afrika-Sana, wafanyabiashara ndogondogo wa soko hilo wameelezea kero inayosababishwa na mifereji inayopitisha maji barabarani kuziba kufuatia uchafu unaotupwa ovyo na hivyo kuelekeza maji katika biashara zao na wateja kukosa sehemu ya 
 
 Vilevile, wafanyabiashara ndongondogo eneo la Ilala-Boma katika soko la Mchikichikini, wamesema mvua zinazoendelea zinawafanya wengi wao kukosa fedha ya kujikimu kutokana na wateja kutokufika kwenye vibanda vyao kwani maji yanajaa sehemu hizo zaq biashara.

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya

                                                                    Fasihi simulizi na Andishi HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAIFA NA HULUTISHI . Utangulizi Fasihi simulizi kwa mujibu wa Mlokozi (1996), ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi inafungamana   na muktadha au mazingira fulani ya kijamii na kutawaliwa na muingiliano wa mambo kama vile Fanani, Hadhira, Fani inayotendwa, Tukio, Mahali pamoja na Wakati wa utendaji.             Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake. Mt...