Skip to main content

FAINALI KOMBE LA FA ARSENAL INATAKA REKODI KWA ASTON VILLA

London,England
ARSENAL leo Jumamosi inacheza fainali yake ya 19 ya Kombe la FA huku ikiwa na rekodi ya kuwa kinara wa kutwaa mara nyingi taji hilo sambamba na Manchester United ikiwa imetwaa mara 11.Klabu hii ya London, kwenye Uwanja wa Wembley inacheza na Aston Villa ya jijini Birmingham.
Mshambuliaji wa Arsenal, Alex Sanchez.


Hadi inafikia hatua ya kucheza fainali, Arsenal iliitoa Reading katika nusu fainali wakati Aston Villa iliitoa Liverpool. Timu zote zilishinda mabao 2-1.

Ikiwa chini ya Kocha Arsene Wenger, Arsenal inataka kuandika rekodi mpya kwa kutwaa mara ya 12 taji hilo na kuiacha Man United ambayo imetwaa mara 11.Arsenal inaingia uwanjani ikiwa ni bingwa mtetezi kwani msimu uliopita ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Hull City mabao 3-2, hivyo kuna kitu ambacho Wenger atataka kukifanya ili kuandika rekodi mpya.

Rekodi zinaweka wazi kwamba, mara ya mwisho Arsenal kutinga fainali ya Kombe la FA na kufungwa ilikuwa mwaka 2001, wakati ilitwaa taji hili kwa mara ya kwanza mwaka 1930 (kumbuka Simba na Yanga zilikuwa bado hazijaanzishwa).
Aston Villa yenyewe imetwaa ubingwa wa Kombe la FA mara saba huku ikicheza fainali mara kumi na kwa mara ya kwanza ilitwaa ubingwa wa michuano hii mwaka 1887 na mara ya mwisho kucheza fainali ilikuwa mwaka 2000 na ikapoteza.

Mara ya mwisho kwa Aston Villa kutwaa ubingwa wa Kombe la FA ni mwaka 1957. Hata hivyo, wakati huu ikiwa chini ya Kocha Tim Sherwood sasa itajitahidi kuweza kutwaa ubingwa huo.

Nyota kama Shay Given, Joe Bennett, Tom Cleverley, Scott Sinclair, Gabriel Agbonlahor, Joe Cole, Fabian Delph, Darren Bent, Charles N’Zogbia na Christian Benteke, watapambana kuhakikisha Aston Villa inatwaa ubingwa.
Mshambuliaji wa Aston Villa, Christian Benteke.
Tofauti na Aston Villa iliyoshika nafasi ya 17 katika msimu uliopita wa Ligi Kuu England, Arsenal iliyoshika nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo, katika fainali hii inaweza kuwakosa nyota wake Theo Walcott, Jack Wilshere na Danny Welbeck ambao ni majeruhi.
Walcott alirejea uwanjani kwa kasi katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England dhidi ya West Brom na kufunga mabao matatu ‘hat trick’ na wengi walidhani angecheza leo lakini kuna shaka ya kujumuhishwa kikosini.  Wilshere, bado anaonekana hayupo vizuri kwani tatizo lake la kifundo cha mguu limechangia kushusha kidogo kiwango chake hivyo kuna shaka ya yeye kucheza leo
Kuhusu wachezaji hao, Wenger anasema: “Sijui nani atakuwa fiti siku hiyo hivyo siwezi kujua nani atacheza au nani hachezi, isipokuwa jambo muhimu kwetu ni kutwaa taji hili siyo kujali nani atakaa benchi na nani atacheza.”
Kuhusu Welbeck ambaye hajacheza tangu aumie katika sare ya bila mabao na Chelsea Aprili 26, mwaka huu na Wenger amesema; “Hatakuwepo, nilijiandaa kwa hilo. Hajafanya mazoezi tangu Ijumaa iliyopita, hivyo nilijua atakosekana katika fainali ya FA.”

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

REALD MADRID YATOKA SARE NA VALENCIA,RONALDO AKOSA PENATI>> Angalia hapa

Cristiano Ronaldo's face tells the story as Real Madrid fail to beat Valencia and leave themselves a near impossible task to catch Barcelona Valencia forward Paco Alcacer celebrates scoring the 19th-minute opener for the underdogs against Real Madrid  Valencia players celebrate their second goal after Javi Fuego heads beyond Iker Casillas from a free-kick Valencia form a huddle as they regroup after taking a 2-0 lead against the side pushing to catch Barcelona in La Liga Ronaldo holds his head in his hand after Real concede their second goal of the match on Saturday evening at the Bernabeu Real Madrid's Javier Hernandez (right) shows his disbelief after missing a golden opportunity to score German midfielder Toni Kroos (right) is upended by Valencia midfielder Andre Gomes during a physical first half Ronaldo signals as Real prepare to restart play after conceded the second goal of the match  Ronaldo steps up for the penalty and a chance to peg one back for his side at 2-0 do...