Mwandishi wetu
Mpasuko! Kufuatia kuibuka wimbi la kashfa za ngono zinazowagusa waseja wa daraja la upadri duniani, baadhi ya waumini wa madhehebu mbalimbali yakiwemo Katoliki na Anglikana, wameibuka na kudai kuwepo kwa marekebisho ya sheria ya makanisa hayo yanayoruhusu watumishi hao kuoa kwani kwa sasa wanayaaibisha, jambo ambalo linaharibu imani juu ya Ukristo.
Hayo yanakuja kufuatia tukio la hivi karibuni la kunaswa kwa Padri Anatoly Salawa ambaye ana cheo cha Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference, Tec) aliyekutwa na mrembo vichakani.
Father Salawa alinaswa na mrembo huyo vichakani ndani ya gari maeneo ya Kurasini jijini Dar.
Mbali na tukio hilo, pia yapo matukio mengine ya mafumanizi likiwemo lile la Father Urbanus Ngowi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi aliyefumaniwa ‘laivu’ na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la mama P.
Katika tukio hilo la mwaka 2013 lililoripotiwa na gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda, Father Ngowi alikutwa na mwanamke huyo ambaye alikuwa muumini wake, chumbani kwake maeneo ya Marangu Wilaya ya Moshi Vijijini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, mwanzoni mwa wiki hii, waumini hao walitolea mifano ya baadhi ya viongozi wa madhehebu hayo kunaswa katika skendo za uhusiano wa kimapenziu hivyo kuona ni bora wakaruhusiwa kuoa ili kuliondolea aibu kanisa.
“Ni bora kama ni sheria irekebishwe ili hawa mapadri waruhusiwe kuoa kwani sasa hii ni aibu kwa kanisa, kuliko kuendelea kuchafua taswira ya misingi ya dini ambayo imekuwepo tangu enzi na enzi.
“Mbona mapadri wengine wa Ulaya Mashariki wa madhehebu ya Katoliki (Ukranian Greek Catholic Church na Coptic Catholic Church) wanaoa? Kwa nini na wa kwetu wasioe?” alihoji mmoja wa waumini hao katika mahojiano na mwandishi wetu ndani ya ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
BARUA YA WAZI KWA PAPA
Mbali na waumini wa hapa nchini, mapema mwaka jana, wanawake wapatao 26 waishio nchini Italia, walimwandikia barua ya wazi Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis wakimueleza mateso wanayopata kwa kuwa na uhusiano wa siri wa kimapenzi na baadhi ya mapadri wa kanisa hilo.
Akifafanua sakata hilo katika mahojiano maalum na Jarida la Republica la jijini Vatikani, Papa Francis alikiri kuwepo kwa taarifa za mapadri kuwa na uhusiano wa kimapenzi, kauli ambayo ilipingwa vikali na msemaji wa kanisa hilo, Federico Lombardi kwa madai kuwa mwandishi wa jarida hilo alimnukuu papa vibaya.
Mbali na hayo, padri mmoja aishiye Italia kutoka Kanisa la Kigiriki la Byzantine lililo chini ya Mamlaka ya Vatican, Jani Pecoraro alisema ifike wakati sasa nyakati zitambuliwe kwani kuoa kwa mapadri hakuondoi weledi wa huduma zao.
“Tunapaswa kusoma nyakati na hakuna shaka kwamba jamii ya sasa imekuwa ikiibua hoja kuwa mapadri waliooa wanaweza kuwa na kiwango sawa cha utumishi na wengine,” alikaririwa padri huyo.
PAPA AWA MAKINI
Hata hivyo, Papa Francis amekuwa makini na jambo hilo huku akieleza kuwa zuio la mapadri kuoa liliasisiwa karne 10, ikiwa ni karne tisa nyuma kabla ya kifo cha Yesu Kristo huku kukiibuka sintofahamu juu ya uamuzi wa papa juu ya mapadri wanaokiuka misingi hiyo.
PIGO KWA KANISA
Mbali na waamini wanaotaka mapadri kuruhusiwa kuoa, wapo wanaoliona jambo hilo kuwa ni pigo jipya kwa kanisa kwani wanatamani mapadri kuendelea kuwa waseja.
“Sisi kama kanisa tutaendelea kusimamia katika misingi ileile ya mapadri kutooa.”
Mpasuko! Kufuatia kuibuka wimbi la kashfa za ngono zinazowagusa waseja wa daraja la upadri duniani, baadhi ya waumini wa madhehebu mbalimbali yakiwemo Katoliki na Anglikana, wameibuka na kudai kuwepo kwa marekebisho ya sheria ya makanisa hayo yanayoruhusu watumishi hao kuoa kwani kwa sasa wanayaaibisha, jambo ambalo linaharibu imani juu ya Ukristo.
Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.
NINI KIMETOKEA?Hayo yanakuja kufuatia tukio la hivi karibuni la kunaswa kwa Padri Anatoly Salawa ambaye ana cheo cha Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference, Tec) aliyekutwa na mrembo vichakani.
Father Salawa alinaswa na mrembo huyo vichakani ndani ya gari maeneo ya Kurasini jijini Dar.
Mbali na tukio hilo, pia yapo matukio mengine ya mafumanizi likiwemo lile la Father Urbanus Ngowi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi aliyefumaniwa ‘laivu’ na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la mama P.
Katika tukio hilo la mwaka 2013 lililoripotiwa na gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda, Father Ngowi alikutwa na mwanamke huyo ambaye alikuwa muumini wake, chumbani kwake maeneo ya Marangu Wilaya ya Moshi Vijijini.
Padri Anatoly Salawa aliyenaswa na binti kichakani.
WAUMINI WAFUNGUKAWakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, mwanzoni mwa wiki hii, waumini hao walitolea mifano ya baadhi ya viongozi wa madhehebu hayo kunaswa katika skendo za uhusiano wa kimapenziu hivyo kuona ni bora wakaruhusiwa kuoa ili kuliondolea aibu kanisa.
“Ni bora kama ni sheria irekebishwe ili hawa mapadri waruhusiwe kuoa kwani sasa hii ni aibu kwa kanisa, kuliko kuendelea kuchafua taswira ya misingi ya dini ambayo imekuwepo tangu enzi na enzi.
“Mbona mapadri wengine wa Ulaya Mashariki wa madhehebu ya Katoliki (Ukranian Greek Catholic Church na Coptic Catholic Church) wanaoa? Kwa nini na wa kwetu wasioe?” alihoji mmoja wa waumini hao katika mahojiano na mwandishi wetu ndani ya ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
BARUA YA WAZI KWA PAPA
Mbali na waumini wa hapa nchini, mapema mwaka jana, wanawake wapatao 26 waishio nchini Italia, walimwandikia barua ya wazi Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis wakimueleza mateso wanayopata kwa kuwa na uhusiano wa siri wa kimapenzi na baadhi ya mapadri wa kanisa hilo.
Mkuu wa Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis.
PAPA ANENAAkifafanua sakata hilo katika mahojiano maalum na Jarida la Republica la jijini Vatikani, Papa Francis alikiri kuwepo kwa taarifa za mapadri kuwa na uhusiano wa kimapenzi, kauli ambayo ilipingwa vikali na msemaji wa kanisa hilo, Federico Lombardi kwa madai kuwa mwandishi wa jarida hilo alimnukuu papa vibaya.
Mbali na hayo, padri mmoja aishiye Italia kutoka Kanisa la Kigiriki la Byzantine lililo chini ya Mamlaka ya Vatican, Jani Pecoraro alisema ifike wakati sasa nyakati zitambuliwe kwani kuoa kwa mapadri hakuondoi weledi wa huduma zao.
“Tunapaswa kusoma nyakati na hakuna shaka kwamba jamii ya sasa imekuwa ikiibua hoja kuwa mapadri waliooa wanaweza kuwa na kiwango sawa cha utumishi na wengine,” alikaririwa padri huyo.
PAPA AWA MAKINI
Hata hivyo, Papa Francis amekuwa makini na jambo hilo huku akieleza kuwa zuio la mapadri kuoa liliasisiwa karne 10, ikiwa ni karne tisa nyuma kabla ya kifo cha Yesu Kristo huku kukiibuka sintofahamu juu ya uamuzi wa papa juu ya mapadri wanaokiuka misingi hiyo.
PIGO KWA KANISA
Mbali na waamini wanaotaka mapadri kuruhusiwa kuoa, wapo wanaoliona jambo hilo kuwa ni pigo jipya kwa kanisa kwani wanatamani mapadri kuendelea kuwa waseja.
Father Urbanus Ngowi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi.
Kuhusiana na sakata hilo, gazeti hili lilikwenda Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kukutana na Katibu wa Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, Denis Aminias na kuzungumza naye ambapo alisema:“Sisi kama kanisa tutaendelea kusimamia katika misingi ileile ya mapadri kutooa.”
Comments
Post a Comment