Messi amwagia sifa staa wa Man Utd
Katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la mtandao wa Shortlist, Lionel Messi, amemtaja staa wa Man Utd, Wayne Rooney, kama miongoni mwawachezaji bora wa Dunia kutokana na kipaji cha hali ya juu alichonacho uwanjani hatakama akihamia ligi kuu nchini Hispania.
Alipoulizwa swali ni kwanini England inashindwa kuzalisha wanasoka bora wenye kiwango cha Dunia alijibu;
‘sidhani kama swala hilo linaukweli juu yake, kwa mfano Rooney ni mchezaji mwenye ubunifu wa hali ya juu nasidhani kama klabu yake ya Man Utd itaweza kumruhusu ahamie katika klabu nyingine kirahisi kutoka na mchango wake katika kikosi.’
Mpaka sasa Rooney ameshafunga magoli 47 katika timu yake ya taifa huku akiifukuzia rekodi Booby Charlton ya magoli 49,
Jumapili hii England itamenyana na Slovenia katika mpambano wa kuisaka tiketi ya kushiriki michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa na Rooney anatazamiwa kupunguza ‘gap’ la magoli mawili anayozidiwa na mkongwe Bobby Charlton.

Comments
Post a Comment