Skip to main content

Wasanii 2 wa Bongo Movie wajiapiza kutozikana>>>Je unajua ni nani....Soma Hapa



Kwa hali ya kushangaza wasanii wawili wa filamu wa hapa nchini William Mtitu na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wamejiapiza kuwa wasizikane ikitokea mmoja kati yao akafariki dunia huku chanzo ni kila mmoja kumtuhumu mwenzake kwa unafiki.

Wakizungumza na Amani kwa nyakati tofauti juzi, wawili hao wameapa wasijuane kwa hali yoyote iwe kwa matatizo kama mmoja wao kufiwa au yeye kufariki dunia, basi mwingine asihudhurie msiba na mazishi ya mwenzake.

Steve Nyerere, ndiye alikuwa wa kwanza ‘kuapa’ mbele ya gazeti hili ndani ya Viwanja vya Leaders, Dar kulikokuwa na kikao cha maandalizi ya sherehe ya harusi ya msanii mwenzao, Hadji Adam ‘Baba Haji’.

“Hakuna mtu mnafiki kama Mtitu, sitaki kabisa hata kumsikia na kila nikimtazama najisikia vibaya mno, mkiwa pamoja anaonekana mwema lakini baada ya hapo anakuwa msaliti, kwanza hata nikifiwa sitaki kumuona msibani, nikifa mimi hakika asihudhurie mazishi yangu, naapa,” alisema Nyerere huku akimtazama mwandishi kwa jicho la ‘sitanii kaka’.

Naye kwa upande wake, Mtitu aliposikia hayo alionekana kumpuuza Nyerere huku akimtolea maneno ya kejeli na dharau kubwa.

“Steve ni mtoto mdogo sana halafu hana elimu kichwani, ameingia kwenye sanaa tunamuona, hana jipya zaidi ya kujipendekeza kwa viongozi wa serikalini kwa kuwaomba hela.

Atafute mtu wa kushindana naye. Hata mimi nikifa asikanyage msibani na kaburini kwangu, nitazikwa hata na mawe au wanyama,” alisema Mtitu kwa sauti iliyojaa jazba na kejeli.

Article Source: Global Publisher

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya

                                                                    Fasihi simulizi na Andishi HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAIFA NA HULUTISHI . Utangulizi Fasihi simulizi kwa mujibu wa Mlokozi (1996), ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi inafungamana   na muktadha au mazingira fulani ya kijamii na kutawaliwa na muingiliano wa mambo kama vile Fanani, Hadhira, Fani inayotendwa, Tukio, Mahali pamoja na Wakati wa utendaji.             Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake. Mt...