Dar es salaam . Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amejitokeza leo na kujibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa wiki moja iliyopita. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Askofu Gwajima amekanusha tuhuma za kuwa alimwambia Dk Slaa kuwa wapo maaskofu ambao walihongwa na mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa na kuitwa mshenga wa mgombea huyo. Askofu huyo amesema kuwa hajawahi kumwambia Dk Slaa kuwa maaskofu wa Kikatoliki wamehongwa na Lowassa ili wamchague hivyo aliyoyasema Dk Slaa ni kuwachafua viongozi hao wa dini. “Dk Slaa anasingizia kuwa maaskofu 30 wamehongwa na Lowassa, hii ni kuwaondolea maaskofu kuaminika (credibility) ili waonekane kuwa hawafai” alisema Gwajima na kuongeza kuwa “ Maaskofu wakatoliki hawakupewa rushwa, maaskofu wa KKKT hawakupewa rushwa, mimi sikupewa rushwa’’ Wakati Dk Slaa anatangaza kustaafu siasa Septemba Mosi, alimwita kiong...