Skip to main content

Video: Matokeo ya Germany vs Georgia na France vs Denmark

Thomas Muller (kulia) akipongezwa na Andre Schurrle (kushoto) baada ya kufunga bao la kwanza
Hapo jana timu ya taifa ya Ujerumani ilipata ushindi mwembamba wa bao 2-1 dhidi ya Georgia katika mechi ya group D na kujikatia tiketi za michuano ya ulaya (Euro 2016) itakayofanyika nchini Ufaransa.


Bao la kwanza lilifungwa na Thomas Muller kwa njia ya penati dakika ya 44 huku la pili likifungwa na Max Kruse dakika ya 78 akipokea pasi ya goli kutoka kwa Mesut Ozil.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa wakimpongeza, Olivier Giroud baada ya kuifungia timu hiyo bao la kuongoza
Wenyeji wa michuano ya hiyo, timu ya taifa ya Ufaransa, ilipata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Denmark yaliofungwa na Straika wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud, katika mchezo uliokuwa wakirafiki.

Comments