Muigizaji wa filamu, Shamsa Ford ameonja joto la jiwe hivi karibuni baada ya kuambulia matusi katika mtandao wa Instagram kutokana na kuvaa kivazi kifupi akiwa mbele ya mtoto wake wa kiume.
Muigizaji huyo mahiri wa filamu ya Chausiku na Bado na Tafuta, ametoa ya moyoni kupitia mtandao huo baada ya kutukanwa na mashabiki.
“Maisha yangu hayawahusu. Ukiona hufulahishwi na chochote toka kwangu ni unfollow. Hukulazimishwa kunifollow. Yaani kuniona kwenye movie ndo mnajifanya mnanijua mpaka mnipangie maisha ya kuishi.sikilizeni nitavaa nitavyojisikia mm hata nikiamua kukaa uchi kabisaa ni mm na wala hayakuhusu. Ww subili movie Itoke ndo unikosoe. Mnaboa sana. Hebu walekebisheni ndugu zenu wanaovaa madila mchana usiku ni vyangudoa,” aliandika Shamsa.
Haya ni maoni ya mashabiki baada ya Shamsa Ford kuweka picha akiwa mevaa nguo fupi mbele ya mwanae.
Salumkiemba218: Angalia huyo mwanao asije akakutamani watoto wa sikuhizi ni shida.
Annmlokole: Tembea uchi bwana unamuogopa nani mbona unavaa?
Hapixlucas: Mmmh waja mwacheni dada wa watu jamani..dnt b so quick to judge her,after all u only see wat she choose to show u! Xo u better get a lyf u mofos…mnakera
Gmassam123Ila: Jaman kuna mambo ya kusifia jaman ila sio kwa uchii huo alio uvaa staa wetu ss hapo ndio unaelimisha nn? jamiii kukupenda tunakupenda sana ila kwa mavazii ya uchi kama hayo waachie wenyewe. Wenye tamadun zao.
Mlimboashura: Huo sio usafi Shamsa wewe ni kioo cha jangu unawafundisha nini wanaokuangalia
Happy.brown001: Duuu….hata kama ni ustaa dear c kwa kujiacha uchi hivyo…hata wazungu now days wana aibu kdg….but am yo fun na.
Comments
Post a Comment