Skip to main content

Man City yapokea dili nono kutoka China


Wamiliki wa klabu ya Man City,  Khaldoon Al Mubarak (kushoto) na Sheikh Mansour (katikati) wameuza hisa 13% za kampuni yao kwa kampuni ya CMC ya China.
Wamiliki wa klabu ya Man City, Khaldoon Al Mubarak (kushoto) na Sheikh Mansour (katikati) wameuza hisa 13% za kampuni yao kwa kampuni ya CMC ya China.
Waswahili wana msemo usemao mwenye nacho huongezewa, msemo huu leo umepata mfano mwingine hai, baada ya moja ya klabu tajiri duniani kutoka EPL kupata dili nono  na kasi ya klabu hiyo ya Manchester City kutaka kuitawala dunia ya soka kuzidi kuimarika.

Kikosi cha Kocha Manuel Pellegrin kinashika nafasi ya kwanza katika EPL baada ya mechi 14.
Kikosi cha Kocha Manuel Pellegrin kinashika nafasi ya kwanza katika EPL baada ya mechi 14.
Klabu hiyo Manchester City leo imetoa tangazo la kuuza sehemu ya hisa za umiliki wa klabu hiyo kwa kampuni ya Kichina, tangazo la City linasema;
‘City Football Group (CFG) leo inatangaza kuunda ushirikiano wa kibiashara na taasisi inayojumuisha wawekezaji wa Kichina ambao wanaongoza vyombo vya habari, burudani, michezo na internet  chini ya kampuni ya CMC (China Media Capital) Holdings.
Klabu za Manchester City, New York City, Melbourne City na Yokohama F. Marinos zote zinamilikiwa na CFG.
Klabu za Manchester City, New York City, Melbourne City na Yokohama F. Marinos zote zinamilikiwa na CFG.
Makubaliano ya kibiashara ya baina ya CFG na CMC Holdings na CITIC Capital yatahusisha uwekezaji wa dola mil 400 ambao utahusisha uamishwaji wa hisa 13% za City Football Group kuwa chini ya CMC. Biashara hii itaifanya kampuni kuwa na thamani ya dola bil 3’
Mwenyekiti wa CMC, Ruigang Li.
Mwenyekiti wa CMC, Ruigang Li.

Kwa kifupi mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour ameuza hisa 13% za umiliki  wake kwa CFG kwenda kwa wawekezaji wa Kichina  ambao wataingiza ndani ya kampuni kiasi cha dola mil 400 (zaidi ya Tsh Bil 800).
Biashara hii inakuja mwezi mmoja baada ya Raisi wa China kuitembelea Manchester City na alionekana akipiga selfie na mshambuliaji Sergio Aguero na waziri mkuu wa UK David Cameroon.
Dili hili ni ushahidi wa kiasi gani Premier League imekuwa sana katika miaka ya karibuni, Mansour alilipa kiasi cha dola mil 400 kuimili kwa asilimia 100% mnamo mwaka 2009 Miaka sita baadae ameuza kiasi cha 13% kwa bei ile ile aliyoinunua klabu nzima.
Hata hivyo, kuna vitu kadhaa bado havipo wazi, ikiwemo ni kiasi gani kitawekezwa katika timu ya Man City tu.
Kampuni ya Sheikh Mansour ya City football group inahusisha vilabu vya Manchester City F.C., Melbourne City FC, New York City FC and Yokohama F. Marinos  na inavyoonekana hivi karibuni atanunua klabu au kuanzisha klabu kwenye ligi ya China.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya

                                                                    Fasihi simulizi na Andishi HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAIFA NA HULUTISHI . Utangulizi Fasihi simulizi kwa mujibu wa Mlokozi (1996), ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi inafungamana   na muktadha au mazingira fulani ya kijamii na kutawaliwa na muingiliano wa mambo kama vile Fanani, Hadhira, Fani inayotendwa, Tukio, Mahali pamoja na Wakati wa utendaji.             Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake. Mt...