Skip to main content

Mhubiri afungwa jela maisha Rwanda





Mahakama Kuu nchini Rwanda imemhukumu kifungo cha maisha jela mhubiri aliyehusika katika mauaji ya kimbari ya 1994.

Jean Uwinkindi alipatikana na hatia ya kupanga na kushiriki katika mashambulio dhidi ya Watutsi, mahakama ilisema.

Mchungaji huyo wa umri wa miaka 64, kutoka jamii ya Wahutu, ndiye mshukiwa wa kwanza wa mauaji ya kimbari kutumwa Rwanda akajibu mashtaka na iliyokuwa mahakama maalum ya UN iliyoendesha shughuli zake kutoka Arusha, Tanzania.

Mahakama hiyo ilifungwa mwezi jana baada ya kuwapata na hatia watu 61 na kuwaachilia wengine 14.

Uwinkindi, aliyekuwa kiongozi wa kanisa la kipentekoste viungani mwa mji mkuu Kigali, alikuwa amepinga kurejeshwa kwake Rwanda.

Alisema hangepata hati Rwanda, ambayo sasa inaongozwa na Watutsi.


Mawakili wake wamesema atakata rufaa uamuzi huo wa mahakama huu. “Mahakama imebaini kwamba kulitokea mauaji ya Watutsi katika milima ya Rwankeri and Kanzenze na mashambulio hayo yaliongozwa na Uwinkindi," alisema Jaji Kanyegeri Timothee, kama alivyonukuliwa na shirika la habari la Reuters.
 Upande wa mashtaka uliambia mahakama kwamba uchunguzi uliofanywa baada ya mauaji hayo uligundua miili 2,000 karibu na kanisa hilo la Kanzenze.

 Uwinkindi alifunguliwa mashtaka 2011 baada ya kukamatwa 2010 katika nchi jirani ya Uganda. Mshukiwa mwingine mkuu, Ladislas Ntaganzwa, alikamatwa wiki mbili zilizopita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

Matokeo ya kidato cha pili mwaka 2015: Zanzibar

MATOKEO YA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI KWA MWAKA 2015 KIWILAYA MJINI MAGHARIBI KUSINI UNGUJA KATI KASKAZINI "A" KASKAZINI "B" MKOANI CHAKE CHAKE WETE MICHEWENI SKULI ZA BINAFSI TANBIHI: KWA UFAFANUZI WA SUALA LOLOTE LINALOHUSU MATOKEO YA MITIHANI TAFADHALI WASILIANA NA OFISI ZA BARAZA LA MITIHANI ZANZIBAR UNGUJA NA PEMBA - AHSANTENI. Source:    Ministry of Education and Vocational Training - Zanzibar Angalia Matikeo ya kidato cha pili bara hapa chini Posted by Maarifa & FIKRA Yakinifu on  Friday, January 15, 2016