Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei kikomo
ya mafuta, ambapo bei ya dizeli imeshuka kutoka Sh. 1,747 hadi Sh
1,600, likiwa ni punguzo la Sh. 147 kwa lita.
Kadhalika,
bei ya mafuta ya petroli imeshuka kwa Sh. 55, hivyo kufanya mafuta hayo
kuanzia leo kuuzwa kwa bei isiyozidi Sh. 1,842 kutoka Sh. 1,898 kwa
lita kama kilivyokuwa ikiuzwa mwezi uliopita.
Taarifa
iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura,
Felix Ngamlagosi, ilieleza kuwa, kupungua kwa bei ya mafuta kwenye soko
la ndani kwa kiasi kikubwa kumetokana na kushuka kwa bei ya nishati
hiyo katika soko la dunia na pia kushuka kwa gharama za usafarishaji na
bidhaa za mafuta hayo kuja nchini.
“Hakukuwa
na mafuta ya taa yaliyoingizwa nchini Januari mwaka huu, hivyo Februari
bei ya bidhaa hii itaendelea kuwa kama ilivyokuwa kwa Januari ambayo ni
Sh. 1,699 kwa lita kwa soko la Dar es Salaam,” alisema.
Ngamlagosi
alisema kushuka kwa namna hiyo kulitokea Machi, mwaka jana, lita moja
ya mafuta ya dizeli ilishuka hadi kufikia Sh. 145 na dizeli kuzwa kwa
Sh. 1,563 kwa lita.
Mkurugenzi
huyo wa Ewura aliwaomba wananchi kupuuza uvumi unaoenezwa kuwa mamlka
hiyo haipendi kushusha bei za mafuta kwa kuwa kushuka kwake kutaadhiri
mapato.
Alisema tozo ya Ewura inatokana na kiasi cha lita za mafuta kinachouzwa na si kupanda kwa bei.
Aidha,
amewakumbusha wamiliki wa vituo vyote vya mafuta kubandika bei za
bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana, yakionyesha bei ya
mafuta, punguzo, vivutio vya biashara na promosheni zinazotolewa na
kituo husika.
Comments
Post a Comment