Ilidaiwa siku ya tukio, Ally alimlawiti mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 16 na kumsababishia maumivu huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Dar es Salaam. Mahakama ya wilaya ya Ilala leo imemhukumu Rizik Ally (25) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kulawiti mvulana wa miaka 16.
Ally ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala amehukumuwa kifungo hicho baada ya mahakama hiyo kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi wanne akiwemo daktari.
Akisoma hukumu hiyo jana, hakimu Flora Haule amesema mahakama yake imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo dhidi ya mshtakiwa huyo.
“Ally ninakuhukumu kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa vijana wengie wenye tabia mbaya kama hii ya kulawiti mtoto wa kiume wakati ukijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria,” amesema hakimu huyo.
Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, wakili wa serikali Ester Kyara aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo.
“Naiomba mahakama hii itoe adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyu kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kulawiti watoto ambavyo huwaletea madhara makubwa watoto hawa ikiwemo kuathirika kisaikolojia,” alidai Kyara.
Awali akisoma hati ya mashtaka, Kyara alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba, 2011 katika eneo la Kariakoo.
Ilidaiwa siku ya tukio, Ally alimlawiti mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 16 na kumsababishia maumivu huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Comments
Post a Comment