Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2016

Watu 580 Wajitokeza Kuhakiki Silaha Dar es Salaam

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imesema watu 574 wamejitokeza kuhakiki wa silaha zao. Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alitoa siku 90 kwa wakazi wa Dar es Salaam wawe wamehakiki silaha zao ifikapo Julai mosi, ikiwa ni miongoni mwa mikakati yake ya kupambana na uhalifu uliokithiri. Hivi karibuni, Rais John Magufuli alihakiki silaha zake anazomiliki. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema wanaendelea kuwahimiza wananchi waendelee kujitokeza kuhakiki silaha zao kwa muda uliotolewa. “Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliokaidi kujitokeza kuhakiki silaha zao, baada ya siku 90 zilizopangwa kumalizika” alisema. Wakati huohuo, Siro alisema wafanyabishara wanaouza vipuri vya magari vilivyotumika maeneo ya Kariakoo, wengi wanauza vilivyoibwa sehemu mbalimbali nchini.  “Nimeshapata mtandao mzima wasipoacha kununua vitu vya wizi tutawakamata na wale wanaojifanya madalali wao, wanashirikiana na majam...

Zitto, Bashe watua Takukuru

*Ni kuhusu tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge *Wahojiwa kwa saa mbili sababu za kujiuzulu kwao OFISI ya Bunge kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), zimeendelea kuwabana wabunge mbalimbali ili kuweza kubaini waliohusika na kupewa rushwa kutoka mashirika ya umma. Kutokana na hatua hiyo, jana wabunge wawili ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, waliitwa kwenda kutoa maelezo Takukuru. Walioitwa jana na kuhojiwa kwa zaidi ya saa mbili ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) na wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM). Licha ya wabunge hao kuwasilisha barua za kujiuzulu kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, kama njia ya kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wenyeviti na makamu wao, lakini bado wamejikuta wakiitwa kama lengo la kusikiliza maelezo yao. Hadi kufikia jana, tayari Takukuru imewahoji zaidi ya wabunge saba, wakiwamo wale wanaotajwa kuhusika na kuchukua mlungula huo pamoja na wale ambao hawajataj...