
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imesema watu 574 wamejitokeza kuhakiki wa silaha zao. 
Mkuu
 wa mkoa huo, Paul Makonda alitoa siku 90 kwa wakazi wa Dar es Salaam 
wawe wamehakiki silaha zao ifikapo Julai mosi, ikiwa ni miongoni mwa 
mikakati yake ya kupambana na uhalifu uliokithiri. 
Hivi karibuni, Rais John Magufuli alihakiki silaha zake anazomiliki. 
Kamanda
 wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema 
wanaendelea kuwahimiza wananchi waendelee kujitokeza kuhakiki silaha zao
 kwa muda uliotolewa. 
“Hatua kali za kisheria zitachukuliwa 
dhidi ya wote waliokaidi kujitokeza kuhakiki silaha zao, baada ya siku 
90 zilizopangwa kumalizika” alisema. 
Wakati huohuo, Siro alisema
 wafanyabishara wanaouza vipuri vya magari vilivyotumika maeneo ya 
Kariakoo, wengi wanauza vilivyoibwa sehemu mbalimbali nchini.
 “Nimeshapata mtandao mzima wasipoacha kununua vitu vya wizi tutawakamata
 na wale wanaojifanya madalali wao, wanashirikiana na majambazi hivyo 
nataka waache mara moja,” alisema. 
Comments
Post a Comment