Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2016

New envoys for deployment abroad

Ms Mindi Kasiga THE Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation plans to deploy 105 staff to foreign embassies and recall 79 others whose tenure has expired. The 79 officials to be returned home include ambassadors, accountants, and other officials, who have retired, or their time in the foreign offices has expired. Addressing journalists yesterday in Dar es Salaam, the Ministry’s Head of Communications, Ms Mindi Kasiga, said Tanzania has 35 embassies in foreign countries, with 234 officers. She explained that the ministry would critically review officers’ terms of references and other requirements to get the kind of people who will be capable of executing duties as outlined by President John Magufuli, which includes representing the country in international meetings. “We are reviewing terms of reference of these ambassadors / officials, before we send them to foreign embassies. We want to send people who have the req...

New Video: Nasi Ft Shaa – Nikilewa

Tazama hapa video mpya ya Dj Nasi wa Iringa amemshirikisha Shaa ngoma inaitwa ‘Nikilewa

Sijawahi kuazima magari ninayo zaidi ya moja – Baraka Da Prince

Msanii wa bongo fleva ambaye anafanya vizuri kwasasa akiongea mna eNewz Baraka Da Prince amekanusha kashfa hizo na kusema kuwa wanaosema anagongea magari ni machizi tu. Zaidi Baraka ameongeza kuwa yeye anamiliki magari zaidi ya moja na hajawahi kuendesha gari ya mtu. Pia Baraka hakuficha kuwa kwa sasa amekwisha mtambulisha msanii mwenzake Naj kwa wazazi wake kuwa ndiye mchumba wake, na amemvisha pete ya ahadi kuwa atakuwa naye milele daima. Alipoulizwa kuwa pete hiyo inamaanisha ana nia ya kumuoa Naj, Baraka alisema “Kwa hilo Mungu ndiye anayejua”.

New Video: Rihanna – She Needed Me, Angalia hapa

Wakati her platinum album “Anti” ikiendelea kufanya vizuri sokoni,Rihanna ameachia new video “Needed Me”.Video hii imekua released ukiwa ni mwezi mmoja umepita tangu alipoachia video nyingine kutoka kwenye album hiyo inayoitwa “Kiss It Better”.

TUCTA Yapinga Mpango wa Rais Magufuli Kukata Mishahara ya Watumishi wa Umma Kutoka Milioni 40 hadi 15 Kwa Mwezi

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta) limepinga mpango wa Rais John Magufuli wa kukata malipo ya mishahara ya watumishi wa umma kutoka Sh40 milioni kwa mwezi hadi Sh15 milioni. Akizungumza na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Kanda ya Ziwa jijini Mwanza jana, Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Hezron Kaaya alisema uamuzi huo ni kinyume na sheria na utaligharimu Taifa iwapo wahusika wataamua kwenda mahakamani kupinga mishahara yao kupunguzwa.  “Watendaji hawa hawakujipangia mishahara wao wenyewe, bali malipo haya yalipangwa na bodi za mashirika na taasisi husika ambazo kisheria zimepewa mamlaka hayo. Malipo haya hayawezi kupunguzwa kwa kauli za kisiasa bila kuzingatia mahitaji ya kisheria,”  alisema. “Iwapo Serikali itatekeleza lengo hili bila kuwapo mjadala mpana na makubaliano ya kisheria kati ya wahusika, basi ijiandae kulipa mamilioni ya fedha kama fidia iwapo watakaokatwa mishahara yao watakwenda mahakamani.” Akiwa mjini Chato wakati wa mapumziko ...

Tangazo la Nafasi ya Kazi.....Anahitajika Administrative Officer

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ateketea kwa Moto Akiwa Ndani ya Gari Lake

Mhadhiri  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta (CoICT), Dk Richard Mgaya amefariki baada ya kuteketea ndani ya gari lake jijini Dar es Salaam juzi. Gari la Dk Mgaya liliteketea baada ya kugongana na lori katika eneo la Mbezi Africana, Wilaya ya Kinondoni usiku wa kuamkia juzi na kuwaka moto uliosababisha kifo chake. Juzi picha mbalimbali zilisambaa zikionesha gari aina ya Toyota Prado lililopata ajali eneo hilo la Africana baada ya kugongana na lori, baadaye ilibainika kuwa aliyekuwa katika gari hilo ni Dk Mgaya. Akizungumza  kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema gari la Dk Mgaya liliteketea na hata kushindwa kujulikana dereva wa gari hilo. Alisema baadaye ndugu wa marehemu ndio walithibitisha kuwa gari hilo lililoteketea na dereva aliyekuwemo ni Dk Mgaya ambaye hata hivyo naye aliteketea ndani ya gari hilo. “Lile gari liliungua na hakuna kitu kilicho...