Msanii wa bongo fleva ambaye anafanya vizuri kwasasa akiongea mna eNewz Baraka Da Prince amekanusha kashfa hizo na kusema kuwa wanaosema anagongea magari ni machizi tu.
Zaidi Baraka ameongeza kuwa yeye anamiliki magari zaidi ya moja na hajawahi kuendesha gari ya mtu.
Pia Baraka hakuficha kuwa kwa sasa amekwisha mtambulisha msanii mwenzake Naj kwa wazazi wake kuwa ndiye mchumba wake, na amemvisha pete ya ahadi kuwa atakuwa naye milele daima.
Alipoulizwa kuwa pete hiyo inamaanisha ana nia ya kumuoa Naj, Baraka alisema “Kwa hilo Mungu ndiye anayejua”.
Comments
Post a Comment