JosƩ Mourinho ndie Meneja mpya wa Manchester United kwa Msimu wa 2016/17 baada ya kusaini Mkataba wa Miaka Mitatu ambao pia unaweza kumuweka hadi Mwaka 2020.
JosƩ, Raia wa Ureno mwenye Miaka 53 na ambae ametwaa Makombe 22 tangu 2003, amefundisha Klabu kadhaa kubwaa Ulaya na kutwaa Mtaji katika Nchi 4 tofauti (Portugal, England, Italy na Spain) ikiwa pamoja na kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI, mara 2 akiwa na FC Porto 2004 na Inter Milan 2010.
Akitangaza rasmi uteuzi huu, Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United Ed Woodward, alisema: “Jose ni Meneja Bora kabisa kwenye Gemu hivi sasa. Ametwaa Mataji na kuhamasisha Wachezaji katika Nchi kadhaa Ulaya na pia anaijua Ligi Kuu England nje ndani ambako ametwaa Ubingwa mara 3! Namkaribisha Manchester United!”
Nae JosĆ© Mourinho amesema: "Kuwa Meneja wa Manchester United ni heshima spesho katika Gemu. Ni Klabu inayojulikana na inayopendwa Dunia nzima. Kuna kitu cha ajabu na mapenzi ambacho Klabu nyingine yeyote hawana!”
Aliongeza: “Siku zote nimekuwa na mvuto mkubwa na Old Trafford, na huu umekuwa ni Uwanja wenye kumbukumbu muhimu kwangu na pia Mashabiki wao tuko vyema. Sasa nina hamu kubwa kuwa Meneja wao na kufurahia sapoti yao kwa Miaka ijayo!”
MOURINHO – WASIFU:
Jina kamili: JosƩ MƔrio dos Santos Mourinho FƩlix
Tarehe ya Kuzaliwa: 26 January 1963 (age 53)
Mahali pa kuzaliwa: SetĆŗbal, Portugal
Klabu alizoongoza kama Meneja:
-2000 Benfica
-2001–2002 UniĆ£o de Leiria
-2002–2004 FC Porto
-2004–2007 Chelsea
-2008–2010 Inter Milan
-2010–2013 Real Madrid
-2013–2015 Chelsea
Mataji aliyotwaa:
FC Porto
-Primeira Liga: 2002–03, 2003–04
-TaƧa de Portugal: 2002–03
-SupertaƧa CĆ¢ndido de Oliveira: 2003
-UEFA Champions League: 2003–04
-UEFA Cup: 2002–03
Chelsea
-Premier League: 2004–05, 2005–06, 2014–15
-FA Cup: 2006–07
-Football League Cup: 2004–05, 2006–07, 2014–15
-FA Community Shield: 2005
Inter Milan
-Serie A: 2008–09, 2009–10
-Coppa Italia: 2009–10
-Supercoppa Italiana: 2008
-UEFA Champions League: 2009–10
Real Madrid
-La Liga: 2011–12
-Copa del Rey: 2010–11
-Supercopa de EspaƱa: 2012
Comments
Post a Comment