Skip to main content

Wadaiwa vyuo vikuu kukamatwa kirahisi

WAKATI serikali ikipanga kuifanyia marekebisho Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Bunge limependekeza wanafunzi wanaonufaika na mikopo hiyo wasipewe vyeti vyao hadi pale watakaporejesha mikopo. 
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dk Joyce Ndalichako akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake Bungeni jana. 

Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17 mjini hapa jana, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolijia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, alisema serikali itaifanyia marekebisho Sheria ya Bodi ya Mikopo ili kuongeza kasi ya urejeshwaji wa mikopo. 

Profesa Ndalichako alisema watalazimika kuifanyia marekebisho sheria hiyo kwa kuwa kiwango cha urejeshwaji wa mikopo bado hakiridhishi. 

Alisema hali hiyo inasababishwa na kuwapo kwa changamoto za kutokuwapo kwa mikakati thabiti ya ufuatiliaji wa wakopaji, udhaifu katika Sheria ya Muundo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kutokuwapo kwa sheria inayolazimisha marejesho ya mikopo kutokana na makato ya mishahara na mwitikio mdogo wa wanufaika kujitokeza kurejesha mikopo yao pamoja na waajiri kutotimiza majukumu yao. 

"Napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wanufaika kufanya marejesho ili Watanzania wengine wenye mahitaji waweze kunufaika. Pia nawasihi wenye uwezo mdogo walipe kwa mkupuo mmoja ili kupunguza utegemezi wa Bodi ya Mikopo kwa serikali," alisema. 

Aliongeza kuwa wizara yake imeongeza siku 30 katika siku 60 zilizokuwa imewapa wanufaika wa mikopo kujisalimisha lakini akaonya kinyume cha hapo majina yao yatatangazwa kwenye magazeti.

Waziri huyo alisema alisema baadhi ya wabunge ni miongoni mwa wadaiwa wa mikopo hiyo. 

Wakati Profesa Ndalichako akitoa rai hiyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo imependekeza wanafunzi wanaopata mikopo ya bodi, baada ya kuhitimu, wawe wanapewa leseni badala ya vyeti. 

Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya bajeti ya wizara hiyo bungeni mjini hapa jana, mjumbe wa kamati hiyo, Hussein Bashe, amependekeza sheria irekebishwe ili wahitimu wawe wanapewa vyeti vyao baada ya kumaliza kurejesha mkopo. 

"Kamati inapendekeza Bodi ya Mikopo iangalie utaratibu wa kutoa leseni badala ya vyeti mara wanafunzi wanapohitimu na vyeti kutolewa mara baada ya kurejesha mkopo kama nchi ya Uingereza inavyofanya," alisema. 

Aliongeza kuwa: "Mbinu hii itasaidia mikopo mingi kurejeshwa kwa wakati na hivyo kuwezesha wanafunzi wengi zaidi kupata mikopo. Kwa kuanzia kamati inashauri kutoa majina yote ya waliokopo magazetini na kupeleka orodha hiyo kwa waajiri wote ili kuwabaini na kuanza kulipa." 

Mbunge huyo wa Nzega Mjini (CCM), pia alisema kamati inapendekeza wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu wapewe vitambulisho vya taifa vinavyoweza kutambulika na benki ili kuhakikisha kila mwanafunzi mwenye kupata mkopo anaunganishwa na Kitengo cha Uratibu wa Mikopo (Credit Reference Bureau) kilichopo Benki Kuu (BoT). 

Alisema utaratibu huo utawezesha kuunganishwa kwa taarifa za mkopaji na benki na taasisi nyingine za fedha, hivyo atalazimika kulipa mkopo kabla ya kupewa mkopo mwingine. 

Bashe alisema kamati hiyo pia inapendekeza serikali iweke idadi kamili ya wanafunzi wanaopaswa kupata mikopo ili bodi ijipange tofauti na utaratibu wa sasa wa kutoa mikopo kwa kuzingatia kiwango cha ufaulu. 

BARAZA LA MITIHANI
Profesa Ndalichako alisema Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) katika mwaka ujao wa fedha litaboresha mfumo wa ukusanyaji na uchakataji takwimu pamoja na kuweka mfumo wa kumtambua mwanafunzi kwa namba maalum ili kuweza kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi husika kutoka anapoandikishwa hadi anapomaliza. 

Waziri huyo pia aliseka baraza litaebdelea kuimarisha utendaji wake kwa kusimika mashine mbili za kufunga bahasha zenye karatasi za mitihani. 

SHERIA YA ELIMU
Waziri huyo pia alisema serikali itafanya mabadiliko ya Sheria ya Elimu ili kuboresha Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kwa ufanisi na wizara yake itakamilisha taratibu za uundwaji wa Bodi ya Kitaalamu ya Walimu. 

BAJETI YA WIZARA
Ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi katika mwaka ujao wa fedha, Profesa Ndalichako aliliomba Bunge liidhinishe Sh. trilioni 1.396. Kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 499.272 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, wakati Sh. bilioni 897.657 zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo. 

HALI YA ELIMU INATISHA
Bashe pia alisema hali ya elimu nchini inatisha na ni hatari kwa uhai na usalama wa taifa. 

Alisema uwezo wa watoto kujifunza kusoma na kuhesabu ni mdogo. Pia miundombinu ya kusomea kama madarasa, mabweni na vyoo haitoshi. 

Ili kutatua changamoto hiyo, Bashe alisema serikali inapaswa kuandaa mpango mkakati wa haraka wa kuhakikisha inatenga bajeti maalum ya kuwezesha miundombinu na idadi ya walimu iongezwe kukabiliana na changamoto ya ongezeko la wanafunzi. 

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

REALD MADRID YATOKA SARE NA VALENCIA,RONALDO AKOSA PENATI>> Angalia hapa

Cristiano Ronaldo's face tells the story as Real Madrid fail to beat Valencia and leave themselves a near impossible task to catch Barcelona Valencia forward Paco Alcacer celebrates scoring the 19th-minute opener for the underdogs against Real Madrid  Valencia players celebrate their second goal after Javi Fuego heads beyond Iker Casillas from a free-kick Valencia form a huddle as they regroup after taking a 2-0 lead against the side pushing to catch Barcelona in La Liga Ronaldo holds his head in his hand after Real concede their second goal of the match on Saturday evening at the Bernabeu Real Madrid's Javier Hernandez (right) shows his disbelief after missing a golden opportunity to score German midfielder Toni Kroos (right) is upended by Valencia midfielder Andre Gomes during a physical first half Ronaldo signals as Real prepare to restart play after conceded the second goal of the match  Ronaldo steps up for the penalty and a chance to peg one back for his side at 2-0 do...