Mtu aliyejeruhiwa akiwa katika gari la kubeba wagonjwa katika uwanja wa ndege wa Ataturk Mwandishi wa VOA Dorian Jones huko Instanbul amesema mlipuaji mmoja wa mabomu alijilipua nje ya eneo la kupokea wageni wa kimataifa kwenye uwanja huo wa ndege eneo hilo kwa kawaida hujaa watu wakingoja usafiri. Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildrim ametoa wito wa umoja wa kitaifa mapema Jumatano asubuhi ikiwa nchi yake inakumbana na ongezeko la vifo kutokana na shambulizi la kujitoa muhanga liliouwa watu 39 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Atartuk -Instanbul huko Uturuki. Yildrim akiwa na mawaziri wake amesema idadi hiyo ya waliofariki ni pamoja na walipua mabomu wa kujitoa muhanga watatu ambao waliwasili na gari aina ya Taxi Jumanne usiku katika uwanja wa ndege ulio na shughuli nyingi na kufyatua risasi kwa kutumia bunduki rashasha na kupiga risasi watu tofauti waliokuwa uwanjani hapo kabla ya kulipua mabomu wakati polisi wakikaribia. Alisema wegi waliuwawa “wengine wako k...
Matukio, Habari za Uhakika