Skip to main content

Mapato bandarini yaongezeka zaidi

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kupungua kwa mizigo bandarini kumeathiri si Tanzania pekee bali dunia nzima na kwamba kubanwa kwa mianya ya wizi kumesababisha kuongezeka kwa mapato kutoka Sh bil 458 Aprili mwaka huu kufikia Sh bil 517.

Aidha, TRA imesema itaanza uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipakodi (TIN) kutokana na kuwepo watu wenye namba mbili na wasiohakiki watalazimika kudaiwa kodi na TRA.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari jana, Kamishna wa TRA, Alphayo Kidata alisema upungufu huo wa mizigo bandarini umezikumba pia bandari za Beira, Msumbiji, Mombasa, Kenya na kwingineko na kusababisha mapato kupungua.

“Lakini sisi pamoja na upungufu wa mizigo bandarini makusanyo yanazidi kuongezeka kutokana na kuzibwa mianya ya kukwepa kodi, hivyo napenda kuwapongeza wafanyakazi wote wa mamlaka na kusema kwa sasa hakuna mtu anayeweza kukwepa kodi na wale waliozoea wakae katika njia kuu,” alisema Kidata.

Kidata alisema wananchi wanatakiwa kuwaunga mkono kwani sasa kodi inaonekana katika kufanya shughuli za serikali kama kuboresha miundombinu pamoja na kutoa elimu bure.

Alisema TRA imefikia na kuvuka lengo la makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2015/16 kwa kukusanya Sh trilioni 13.8 sawa na asilimia 100.04 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 13.4 iliyokuwa imepangwa na serikali.

Kidata alisema katika kipindi cha Juni mwaka huu, TRA imekusanya Sh trilioni 1.4 sawa na asilimia 107.83 ya lengo la kukuzanya Sh trilioni 1.3 ambapo makusanyo ya mwaka wa fedha 2015/16 ni sawa na ongezeko la asilimia 23.70 la makusanyo ya mwaka 2014/15.

Akizungumzia mashine za kielektroniki za EFDs, Kidata alisema walipoanza utoaji mashine hizo zilikuwa 5,703 na mpaka sasa mashine 1,700 zimegawiwa kwa watumiaji na wataanza kupita duka hadi duka kuhakiki matumizi ya mashine hizo.

Kamishna wa mapato ya ndani, Elijah Mwandumbya, alisema mwaka huu wa fedha wamejipanga kuhakikisha wanaondoa changamoto kwa mtu mmoja kuwa na TIN zaidi ya moja hivyo watafanya uhakiki.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIE MWANAUME"[SHOGA] MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI,KAAMUA KUPOST HIZI PICHA INSTAGRAM.

Kutana na mwanaume mwenye makalio makubwa kama mwanamke.Kwa jina anaitwa Micah,ni mwanaume ambaye hipsi na makalio yake zinazidi hata zile za wanawake huwezi kuamini hebu tazama hapa utakubali tu mwenyewe.

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015 YOTE HAYA HAPA

Angalia yote hapa NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2015 EXAMINATION RESULT ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA KILIMANJARO LINDI MARA MBEYA MOROGORO MTWARA MWANZA PWANI RUKWA RUVUMA SHINYANGA SINGIDA TABORA TANGA MANYARA GEITA KATAVI NJOMBE SIMIYU   

Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya

                                                                    Fasihi simulizi na Andishi HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAIFA NA HULUTISHI . Utangulizi Fasihi simulizi kwa mujibu wa Mlokozi (1996), ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi inafungamana   na muktadha au mazingira fulani ya kijamii na kutawaliwa na muingiliano wa mambo kama vile Fanani, Hadhira, Fani inayotendwa, Tukio, Mahali pamoja na Wakati wa utendaji.             Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake. Mt...