Wapiganaji kutoka moja ya makundi yanayopigana kwenye mji wa Kidal,Mali |
Kundi la wanamgambo la Tuareg linaloungwa mkono na Serikali linasemekana kuchukua udhibiti wa mji wa kaskazini wa Kidal nchini Mali.
Kundi la wanamgambo la Tuareg linaloungwa mkono na Serikali linasemekana kuchukua udhibiti wa mji wa kaskazini wa Kidal nchini Mali, baada ya mapigano kuzuka na kundi lilioundwa na watu waliokuwa waasi wa Tuareg.
Mtu alieshuhudia aliambia VOA idhaa ya Kifaransa kuwa wapiganaji wa Gatia walikuwa wakifanya msako kwenye mji huo Alhamisi jioni ili kuwasaka waasi waliojificha.Hata hivyo hali mjini humo ingali haieleweki na haijabainika kama kuna majeruhi wowote.
Kiongozi wa muungano wa Tuareg Ambeyri Ag Rissa,ameambia maafisa wa VOA kuwa alikuwa akitoka kwenye mkutano kuhusu uuwiano uliotiwa saini Jumapili kuhusu ugavi wa udhibiti kwenye mji huo baada ya mapigano kuzuka. Milio ya risasi ilisikika nyuma yake wakati akizungumza.
Hali mjini humo imebaki kuwa tete hata baada ya mkataba huo kutiwa saini huku pande zote zikilaumiana kwa kuzuka tena kwa mapigano