Yanga Bingwa 2015/2016!! Hizi ni baadhi ya headlines kwenye kurasa za michezo.. haikumaanisha kwamba matokeo ya mwisho yalikuwa yameamua hivyo, ila wanaspoti walipiga hesabu ya pointi ambazo yatari YANGA walikuwa wamejikusanyia mpaka mechi yao ya mwisho, hii ya leo ambayo Yanga wamekutana na Polisi Morogoro tayari imetoa matokeo. Yanga imefikisha jumla ya pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki ligi kuu msimu huu, kwa matokeo hayo basi Yanga wanakuwa mabingwa wa Ligi hiyo. Mechi hiyo kati ya Yanga na Polisi Moro ilikuwa ikipigwa katika Uwanja wa Taifa Dar.. mechi imekamilika kwa Yanga kutoka kifua mbele kwa goli 4-1. Hamis Tambwe leo aliweza kuing’arisha Yanga baada ya kupachika magoli matatu ambapo goli la kwanza alifunga dakika ya 40 kufuatia krosi ya Saimon Msuva, goli la pili alilifunga dakika ya 53 na goli la mwisho alifunga baada ya kupokea cross kutoka kwa Mrisho Ngassa. Msuva alikamilisha idadi ya mabao kwa kupiga bao la nne ambapo baadae ...
Matukio, Habari za Uhakika