Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2015

PICHA za kutoka ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Mbunge Edward Lowassa awavuta watu wengi kumsikiliza

Niko karibu na wewe mtu wa nguvu.. Headlines nyingi kwenye vyombo vya habari ni ishu ya Uchaguzi Mkuu TZ 2015, wagombea nao kila mmoja anachukua headlines zake! Niko ndani ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Arusha ambako anasubiriwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa, kaahidi kuongea kitu leo.. ninakusogezea kila kinachoendelea mtu wangu, haupitwi na chochote ukiwa karibu na millardayo.com. Mahema ya huduma ya dharura yamewekwa katikati ya Uwanja tayari. Moja ya geti kubwa la watu kuingilia Uwanjani. Ukaguzi unaendelea pia kwa kila anaeingia Uwanjani kuhakikisha tu Usalama unakuwepo. Mabango nayo hayajaachwa yani !

Soma Magazeti ya Tanzania na stori zote za leo May 30 2015

WAUMINI: MAPADRI WARUHUSIWE KUOA

Mwandishi wetu Mpasuko! Kufuatia kuibuka wimbi la kashfa za ngono zinazowagusa waseja wa daraja la upadri duniani, baadhi ya waumini wa madhehebu mbalimbali yakiwemo Katoliki na Anglikana, wameibuka na kudai kuwepo kwa marekebisho ya sheria ya makanisa hayo yanayoruhusu watumishi hao kuoa kwani kwa sasa wanayaaibisha, jambo ambalo linaharibu imani juu ya Ukristo. Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo. NINI KIMETOKEA? Hayo yanakuja kufuatia tukio la hivi karibuni la kunaswa kwa Padri Anatoly Salawa ambaye ana cheo cha Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference, Tec) aliyekutwa na mrembo vichakani. Father Salawa alinaswa na mrembo huyo vichakani ndani ya gari maeneo ya Kurasini jijini Dar. Mbali na tukio hilo, pia yapo matukio mengine ya mafumanizi likiwemo lile la Father Urbanus Ngowi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi aliyefumaniwa ‘laivu’ na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la mama P. Katika tukio hi...

FAINALI KOMBE LA FA ARSENAL INATAKA REKODI KWA ASTON VILLA

London,England ARSENAL leo Jumamosi inacheza fainali yake ya 19 ya Kombe la FA huku ikiwa na rekodi ya kuwa kinara wa kutwaa mara nyingi taji hilo sambamba na Manchester United ikiwa imetwaa mara 11.Klabu hii ya London, kwenye Uwanja wa Wembley inacheza na Aston Villa ya jijini Birmingham. Mshambuliaji wa Arsenal, Alex Sanchez. Hadi inafikia hatua ya kucheza fainali, Arsenal iliitoa Reading katika nusu fainali wakati Aston Villa iliitoa Liverpool. Timu zote zilishinda mabao 2-1. Ikiwa chini ya Kocha Arsene Wenger, Arsenal inataka kuandika rekodi mpya kwa kutwaa mara ya 12 taji hilo na kuiacha Man United ambayo imetwaa mara 11.Arsenal inaingia uwanjani ikiwa ni bingwa mtetezi kwani msimu uliopita ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Hull City mabao 3-2, hivyo kuna kitu ambacho Wenger atataka kukifanya ili kuandika rekodi mpya. Rekodi zinaweka wazi kwamba, mara ya mwisho Arsenal kutinga fainali ya Kombe la FA na kufungwa ilikuwa mwaka 2001, wakati ilitwaa taji hili kwa mara ya kwanza...