MWANASIASA mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, jana kwa mara ya kwanza alipanda jukwaani kumnadi mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na kusema mabadiliko ni lazima. Kingunge aliyasema hayo jijini Arusha kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Sinoni. Kingunge alihutubia huku mvua ikinyesha, lakini wananchi waliokuwa eneo hilo hawakuondoka. βHistoria yangu, nimeshiriki katika kuleta mabadiliko na ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kwamba kwa sasa mabadiliko katika Tanzania ni lazima, sisi t umekuwa huru kwa miaka 54 sasa. βTulivyounda Tanu tulitaka chombo cha mabadiliko na Zanzibar walivyounda Afro Shirazi walitaka kuwakomboa Waafrika wenzao, vyama vyote viwili vilitaka Watanzania tupate mabadiliko na baadaye kwakuwa waliamini katika mabadiliko, waliunganisha vyama na baadaye nchi, na mimi nilikuwa kwenye kamati ya watu 20 kuanzisha CCM. βCCM katika miaka ya karibuni kimekuwa na dalili ...